SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, June 14, 2011

Benki Ya KCB Tanzania Yaadhimisha Siku Ya Mazingira Kwa Kupanda Miti

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakimwagilia maji katika moja ya mti waliyopanda wakati wa wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na mazingira duniani uliofanyika katika Kijiji cha Msongola  Chanika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Benki ya KCB Tanzania Christine Manyenye akiwaongoza wafanyakazi wenzake kupanda miti  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na ya mazingira duniani iliyofanyika katika  Kijiji cha Msongola, Chanika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania Edmund  Mndolwa (Kushoto) akimwagilia maji mti alioupanda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na mazingira duniani uliofanyika katika Kijiji cha Msongola Chanika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB  Tanzania Christine Manyenye.
Diwani  wa Kata ya Msongola Angela Malembeka  akipanda mti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na mazingira duniani uliofanyika katika Kijiji cha Msongola  Chanika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Moezz Mir na katikati  ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Christine Manyenye.
Wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakigawa juisi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Msongola walioshiriki uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 21,000 kuadhimisha siku ya jamii na mazingira duniani uliofanyika katika Kijiji cha Msongola  Chanika jijini Dar es Salaam.  

0 comments:

Post a Comment