SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, June 15, 2011

VODACOM FOUNDATION YAENDELEA KUWAJALI WANAWAKE NA WATOTO!!

Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba katikati akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba  wa shilingi Milioni 40, zilizotolewa na Vodacom Foundation kwa CCBRT kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto katika hospitali mpya ya CCBRT Boabab. Kushoto Afisa Mtendaji Mkuu wa  CCBRT  Erwin Telemans,watatu toka kushoto Meneja Mahusiano wa CCBRT Kira Thomas na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans kushoto, Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba wakisaini makubaliano ya Vodacom Foundation kuchangia shilingi Milioni 40 za ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto kwenye Hospitali mpya ya CCBRT Boabab itakayojengwa jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia katikati Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na kulia Meneja Mahusiano wa CCBRT Kira Thomas.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans kushoto  akipokea  mkataba  kutoka kwa Afisa Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makambawa Vodacom kwa ajili ya  kuchangia shilingi milioni arobaini katika ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto kwenye hospitali maalum ya wanawake  itakayojengwa jijini Dar es salaam.Kulia ni Meneja Mahusiano wa CCBRT Kira Thomas .
Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba (kulia) Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule wakimwangalia  Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans (kushoto) akisoma mkataba wa makabadhiano ya shilingi Milioni Arobaini kutoka Vodacom zitakazotumika katika ujenzi wa jengo la wanawake na watoto katika Hospitali ya CCBRT Baobab.

0 comments:

Post a Comment