SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, May 7, 2011

TUZO ZA WANAMICHEZO 2010 BORA ZAFANA

Mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo bora mwaka 2010 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa hotuba kwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Movenpick jijini Dar usiku wa kuamkia jana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za wanamichezo bora 2010, Masoud Saanan akizungumza katika hafla  hiyo.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Ghari Bilal wakifurahia jambo na Mh. Benjamin Mkapa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin Mkapa tuzo maalum ya heshima kutokana na mchango wake katika sekta ya michezo hasa kufankikisha ujenzi wa uwanja mpya wa taifa wakati wa utawala wake.
Mh. Benjamin Mkapa akionyesha tuzo hiyo kwa wageni waliohudhuria hafla hiyo ukumbini hapo.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin Mkapa akimpatia tuzo yake Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL,Teddy Mapunda mara baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal usiku wa kuamkia jana katika hoteli ya Movenpick jijini Dar.
Mh. Benjamin Mkapa akizungumza  wakati akitoa shukrani kwa tuzo maalum aliyoipata kwa mchango wake sekta ya michezo. Tuzo hiyo iliyotolewa na Chama cha Michezo nchini TASWA. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za wanamichezo bora 2010 Masoud Saanan.
Vijana wa THT wakitoa burudani katika hafla hiyo.
Mchezaji wa Timu ya Netiboli ya Mbweni JKT Mwanaidi Hassan (kulia) akipewa tuzo na Mgeni rasmi Dkt. Mohamed Gharib Bilal baada ya kuibuka kuwa mwanamichezo bora wa mwaka 2010 pamoja na kupewa zawadi ya gari aina ya Toyota Crester. Kutoka kushoto ni Operation Manager wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo pamoja na Waziri Emmanuel Nchimbi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bi. Balndina Nyoni akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Magazeti ya Guardian Limited Bw. Kiondo Mshana katika hafla hiyo.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akikabidhi tuzo ya mwanamichezo bora wa Tanzania aliyopo nje  Hasheem Thabit (hayupo nchini) ikipokelewa na mama yake mzazi.
Mwenyekiti wa Chama cha Michezo nchini Juma Pinto akikabidhi tuzo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Habari leo Hussein Bashe akikabidhi tuzo.
 
 
Operation Manager wa Multichoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akimkabidhi Mwanamichezo bora wa mwaka 2010 Mwanaidi Hassan Decorder full set ya DStv ambayo imelipiwa kwa miezi mitatu.
Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi funguo za gari mwanamichezo bora wa mwaka 2010 Mwanaidi Hassan.

Mwanaidi Hassan akifurahi mara baada ya kukabidhiwa funguo.
Mwanaidi Hassan akijaribu gari lake mara baada ya kukabidhiwa.

0 comments:

Post a Comment