SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, May 15, 2011

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na  Michezo Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi (Mb), atakutana na wasanii katika ukumbi wa  BASATA kuanzia tarehe 17 Mei na tarehe 18 Mei, 2011.
 Waziri ataongea na wasanii kwa  utaratibu ufuatao:-

 17/05/2011 (Jumanne) Saa 4:00  asubuhi   Wasanii Wote wa Sanaa za Muziki 
18/05/2011 (Jumatano) Saa 4:00  asubuhi  Wasanii Wote wa Sanaa za Ufundi,Filamu na  Maonyesho.
Izingatiwe kwamba Waziri ataongea na  wasanii wa muziki wa aina zote wakiwemo wa Kizazi kipya,Bendi,Disco,  Asili,Taarab na kadhalika katika siku ya kwanza.Katika siku ya pili yaani  Tarehe 18/05/2011 ataongea na wasanii wa Sanaa za Filamu,Maonyesho na  Ufundi pekee.
 Wasanii Wote mnaombwa kujitokeza kwa  wingi.

 Lengo kuu la mikutano hii kati ya  Waziri na Wasanii ni kuongelea maendeleo ya fani za  sanaa.

 Ghonche Materego.
KATIBU MTENDAJI.

0 comments:

Post a Comment