SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, May 15, 2011

BAFANA BAFANA YAICHAPA TAIFA STARS BAO 1-0

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, muda mfupi kabla ya pambano dhidi ya Bafana Bafana ya Afrika Kusini jana , mchezo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Picha na Mdau Richard Mwaikenda
Timu ya soka ya Taifa,Taifa Stars imeshindwa kutamba mbele ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa 
Dar es Salaam.
Wageni walipata bao katika dakika ya 43 mfungaji akiwa Siyabonga Sangweni aliyefunga bao hilo kwa kichwa kutokana na mpira wa kona ambao uzembe wa kipa wa Stars, Juma Kaseja na beki yake, ulifanya washindwe kuokoa.
Kwa habari zaidi: 

0 comments:

Post a Comment