SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 17, 2011

MUSEVENI AZUNGUMZA NA WANADIPLOMASIA WA KIGENI KUHUSU BESIGYE

Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekutana na kuzungumza na wanadiplomasia wa kigeni wanaowakilisha nchi na mashirika ya nje nchini Uganda na kuwataka kutomuunga mkono kiongozi wa kisiasa nchini humo Dk. Kiiza Besigye.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu ya Entebbe na kuhudhuriwa na zaidi ya wanadiplomasia 50  kutoka Afrika, Umoja wa Ulaya (EU), Asia na Marekani, rais Museveni amesema kiongozi huyo wa upinzani anafanya vitendo vya utovu wa nidhamu na vinavyo kwenda kinyume cha sheria.
Museveni amewaelezea kuwa wakati wa kurejea kwa kiongozi huyo kutoka Nairobi alikwenda kupata matibabu, polisi walikubaliana kuwa msafara wa Besigye ungetumia barabara ya Kampala-Entebbe kwa muda wa saa moja.
Lakini badala yake kiongozi huyo wa upinzani alitumia saa 10, kitendo ambacho kilisababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara hiyo, wakiwemo wakuu wan chi waliokuwa wakiwasili nchini humo wakitumia barabara hiyo walikuwa wanakwenda kuhudhuria sheria za kuapishwa kwa rais Museveni.
Amesema tabia za namna hiyo hazitaweza kujenga demokrasia nchini Uganda na serikali haiku tayari kupoteza demokrasi iliyopo nchini humo.

0 comments:

Post a Comment