SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 17, 2011

MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL ZIARANI MKOA WA KASKAZINI PEMBA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanafunzi wa Shule ya Msingi Simai iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka  jiwe la msingi katika , Shule ya Msingi Simai iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwa kwenye Ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Miikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.
(Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais)

0 comments:

Post a Comment