Mama Balozi Joyce Kallaghe akimkaribisha mgeni rasmi Mama Tunu Pinda.
Mgeni rasmi Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiongea na wakina mama.
Mke wa Balozi wa Kenya akisalimia wakina mama.
Mariam Mungula na Mama Pinda.
Mjumbe wa NEC Asha Baraka akiwa na Jestina.
Wakina Mama katika pose na mgeni rasmi.
Wakina mama katika picha ya pamoja.
Mrs. Agnes Atim Apea – Motivation Speaker, PhD Student, Gender and HIV, Reading University; Dr. Bunmi Arogunmat – Motivation Speaker; Terrence Higgins Trust,Mama Balozi, Tanzania; Mama Waziri Mkuu, Tanzania; Dr. Sylvia Anie, Director, Social Transformation Programmes Division, Commonwealth Secretariat, Sponsors of the prommmae and Mama Balozi, Kenya.
*************************************
YALIOYOJIRI SEMINA YA WAKINA MAMA NCHINI UINGEREZA TAREHE 21 MAY 2011.
TA-UK ikishirikiana na TAWA waliandaa semina ya akina mama iliyofanyika:
Nyumbani kwa Balozi wa Tanzania Uingereza, Jumamosi, 21 Mei 2011.
Mgeni Rasmi alikuwa Mama Pinda Mke wa Waziri Mkuu, Tanzania.
Mada ya
Semina ilikuwa “Wanawake kama Wakala wa Mabadiliko” na mkazo zaidi
kwenye – Mwamsho kuhusu Waafrika waishio Uingereza wanaoishi au walio
adhirika na UKIMWI” “HIV and AIDS Awareness Seminar: for African
communities affected by HIV and AIDS in the United Kingdom.
Kusudio na Mategemeo ya Semina:
Makusudi ya
semina yalikuwa: kuwakumbusha/mwamko kuhusu Ukimwi, kuzungumzia maswala
ya stigma, ubaguzi, watu kutokukubali (denial), kukubali na kuweza
kujitokeza. Inategemewa hatimayekuweza kuwa na vikundi vya kusaidiana
baini ya Waafrika hususani Watanzania waishio Uingereza.
Objectives:
The seminar
aims to: Raise HIV and AIDS awareness, discuss issues of stigma,
discrimination, denial, acceptance and disclosure of HIV status,
training needs, develop support and social network groups among the
African communities living in the UK.
Semina ilikuwa katika sehemu mbili:
Sehemu ya kwanza ilikuwa kwa Kiingereza na wazungumzaji wakuu walitoa changamoto kuhusu:
1.Akina
Mama kama Wakili wa Mabaliko: Akina mama walikumbushwa kwamba afya ni
jambo la mhimu kwa kila mtu. Maendeleo au mabadiliko yeyote yale yana
leletwa na watu wenye afya nzuri. Kwa hiyo ni vema mama kujali afya
yako ikiwa ni pamoja na kuungalia mwili wako kama vile kwenda hospital
na kupimwa kwa magonjwa mbali mbali, kubadilisha mwenendo wako. Mama
akiweza kujali na kubadilisha mwenendo wake yeye atakua mfano na kuwa
taa kwa watu waliokaribu naye – familia pamoja na jamii kwa ujumla.
2.Kuishi
kwa mategemeo –“Living positively with HIV” – Hii ilikuwa changamoto
sana kwa wajumbe, watu walielezwa kuwa ukiwa na UKIMWI siyo mwisho wa
maisha. Mtoa mada kwanza aliuza swali hivi nani anaweza kumtumbua mtu
aliyeaidhirika kwa Ukimwi yuko vipi au unaweza kumtambua vipi? Jibu
hakuna mtu ambaye anaweza kutambua labda mtu akiwa mahututi kitandani.
Jibu ni kwamba mtu ye yote Yule anaweza kuwa ana Ukimwi lakini hakuna
anayejua. Mtoa mada alisema kuwa yeye ameadhirika tangu akiwa mdogo
lakini sasa hivi ameolewa na ana watoto. Amesoma na anafanya PhD na
anaishi maisha ya furaha kama watu wote. Fundisho jamani ukiwa na UKIMWI
siyo mwisho wa maisha. Lakini unaweza kufanikiwa kuishi haya maisha
kama utapimwa na ikajulikana mapema kuwa umeadhirika ili ukapata msaada.
Sehemu ya pili:
Mama Balozi
alimkaribisha Mama Waziri Mkuu. Mama Pinda alisema kuwa amefurahishwa
sana na kitendo cha akina mama kukutana na kuwa na semina nzuri sana
iliyoelimisha, kufumbua watu kuelewa mambo zaidi. Vile vile alimshukuru
Mama Balozi kwa kuweza kuwakaribisha wanawake nyumbani kwake.
Aliahidi kuwa endapo atapata nafasi ya kuja Uingereza tena atajihidi kukutana na akina mama. Semina za uamusho kwa
Vile vile
wakati huu wajumbe walipata nafasi ya kupata changamoto nyingine toka
kwa mtu ambaye vile vile amejitokeza kuwa yeye ameadhiriwa na Ukimwi,
alisema siyo jambo rahisi kujitokeza kwani kuna mambo mengi sana kama
vile– dharau, kukataliwa na ndugu, kuogopa kuondolewa etc. Alisema
ameweza kufika hapa kwa sababu alitambua mapema kuwa ameadhiriwa. Kwa
hiyo changomoto ilikuwa jamani
tujitahidi kupimwa mara kwa mara.
Kusudu na Mategemeo ya Semina:
Makusudu ya
semina yalikuwa: kuwakumbusha/mwamko kuhusu Ukumwi, na kuzungumzia
maswala ya stigma, ubaguzi, watu kutokukubali (denial), kukubali na
kuweza kujitokeza na na hatimaye kuweza kuwa na vikundi vya kusaidiana
baini ya Waafrika hususani Watanzania waishio Uingereza.
TA-UK
itaendelea kuandaaa hizi semina kwa kushirikiano na vikundi mbali mbali
vya Kitanzania, Africa Mashariki vilivyop nchini Uingereza. Hizi Semina
zinadhaminiwa na msaada kutoka Commonwealth Secretariat.
0 comments:
Post a Comment