SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 10, 2011

MAKAMU WA RAIS, WAZIRI WA ARDHI WAHUDHURIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA ISTANBUL

 Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiingia kwenye Ukumbi wa Mkutano wakati aliwasili kwenye ukumbi huo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya Nchi masikini Duniani. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika Mei 13 mwaka huu, jijini Istanbul Uturuki.
 Makamu wa rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mahadhi Maalim walipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi masikini unaoendelea Jijini Istanbul Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika  Mei 13 mwaka huu.
 
 Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika chumba cha mkutano alipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi masikini Duniani, unaoendelea jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajia kumalizika Mei 13 mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Dkt. Anna Tibaijuka akiwa na Waziri wa Ofisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyihaji Makame (katikati) na Mbunge wa Kigamboni, Dar es Salaam, Dkt. Faustine Ndugule wakiwa ndani ya ukumbi wa mkutano wakati walipohudhuria mkutano wa umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya nchi masikini Duniani, unaoendelea jijini Istanbul, Uturuki. Mkutano huo ulianza jana Mei 9 na unatarajiwa kumalizika Mei 13 mwaka huu. 
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

0 comments:

Post a Comment