SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, May 22, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA NA KUKAGUA KILIMO CHA UMWAGILIAJI BONDE LA MPUNGA BUMBWISUDI!!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongozana na viongozi wa CCM wakati alipofika Wilaya ya Magharibi kwa ajili ya kukagua matengenezo ya Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi Zanzibar jana Mei 21.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM, wakati alipofika Wilaya ya Magharibi kwa ajili ya kukagua matengenezo ya Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi Zanzibar jana Mei 21.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya jingo la Ofisi ya  CCM, wakati alipofika Wilaya ya Magharibi kwa ajili ya kukagua matengenezo ya majengo ya Ofisi hiyo ya CCM iliyopo  wilayani hapo,  akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi Zanzibar jana Mei 21.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Affan Othman (wapili kulia), wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji wa Mpunga katika Bonde la Mpunga la Bumbwisudi lililopo eneo la Popo Jimbo la Dole Unguja mjini Zanzibar jana Mei 21.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa mabonde ya Mpunga ya Bumbwisudi, Kadili Ali ( kulia), wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji wa Mpunga katika Bonde la Mpunga la Bumbwisudi lililopo eneo la Popo Jimbo la Dole Unguja mjini Zanzibar jana Mei 21.
Baadhi ya wanachama wa CCM na wananchi wa Mwera Misufini Mkoa wa mjini Magharibi, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal, alipofika wilayani hapo jana Mei 21 kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika Jengo la Ofisi ya CCM Tawi la Mwera Misufini. 
Wasanii wa kughani, Dodo Rajab (kushoto) na Amina Mohamed, wakitoa burudani ya kusoma utenzi mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, 
alipofika kuweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya CCM Tawi la Misufini Mkoa wa mjini Magharib jana mei 21.
Baadhi ya wanachama wa CCM na wananchi wa Mwera Misufini Mkoa wa mjini Magharibi, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal, 
alipofika wilayani hapo jana Mei 21 kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika Jengo la Ofisi ya CCM Tawi la Mwera Misufini.
(Picha na Muhidin Sufiani-OMR).

0 comments:

Post a Comment