SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, May 24, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA WARSHA YA SIKU MBILI KUHUSU UTAFITI YA VYUO VIKUU!!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi. Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25.   

Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipokuwa akifungua warsha hiyo leo.  


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal  akisalimiana na Profesa Amandina Lihamba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kufungua Warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi. Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na washiriki baada ya kufungua rasmi warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi. Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25
(Picha na Muhidin Sufiani-OMR).

0 comments:

Post a Comment