Umati wa waandamanaji mkoani Mbeya juu na chini.
Hivi karibuni CHADEMA imefanya maandamano yaliyowashirikisha wakazi wa mji wa Mbeya, maandamano yaliyoongozwa na viongozi wa ngazi ya juu kitaifa kwa lengo la kuishinikiza Serikali iachane na mambo kadhaa, ikiwamo muswada wa kubadilisha Sheria ya Ununuzi wa Umma ili kuruhusu ununuzi wa vitu chakavu, mchakato wa katiba uondolewe mikononi mwa CCM, kuunganisha nguvu ya umma ili kupinga bidhaa kupanda bei na kutaka uchaguzi wa Meya wa Arusha ufanyike upya.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa alisema lazima Serikali ishushe bei ya sukari na mafuta, "Haiwezekani wanavuana magamba halafu wananchi wanaendelea kuteseka. Magamba ni yao, wananchi waangaliwe, ...tunawahamasisha Watanzania kuangalia hali ya maisha yao kwa sababu ni haki yetu ya msingi, na tunataka wananchi waionyeshe Serikali yao mambo yanayowasumbua" - Dk Slaa.
Mwenyeiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema chama hicho kitapinga ongezeko la kodi yoyote bungeni katika bajeti ijayo mpaka kieleweke na kwamba Serikali isipofanya hivyo watapigana bungeni kwa maslahi ya wananchi. Akasema kuwa ongezeko la kodi linawaumiza wananchi na Serikali imekaa kimya wakati hali ya maisha inaendela kuwa mbaya, "Wabunge wa CHADEMA tutaendelea kukomaa mpaka kieleweke kwa kuwa hatuvunji amani, bali tunawahangaikia wananchi ili wawe na maisha bora," "...kama Serikali inataka kuona uwezo wetu wa kuhamasisha Watanzania wapandishe kodi katika bajeti ya mwaka huu..." - Mbowe.
Wakati wa kufungua tawi la chama hicho katika chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU), kabla ya maandamano hayo kuanza, Dk. Slaa alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa kuacha kuvitisha vyama kwa barua kuwa visifungue matawi vyuoni, "Tendwa ajue kuwa wanafunzi nao ni wananchi na ajue kuwa sisi kama Chadema tunafuata taratibu, hivyo asitutishe," - Dk. Slaa.

0 comments:
Post a Comment