SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 16, 2011

NIGERIA WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS

Wananchi nchini Nigeria leo wanapiga kura katika uchaguzi wa rais wa taifa la kwanza kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha People’s Democratic (PDP) anachuana vikali na Meja Jenerali Mstaafu Muhammadu Buhari wa Congress for Progressive Change (CPC), Nuhu Ribadu wa Action Congress of Nigeria (ACN) na Ibrahim Shekarau wa All Nigeria People’s Party (ANPP).

Buhari na Ribadu wanaonekana kutoa upinzani mkali kwa Rais Jonathan, lakini huenda rais huyo akashinda kwa kiwango kidogo.

Buhari aliwahi kuwa rais aliyeingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 1983 kabla nayeye kupinduliwa na Jenerali Ibrahim Babangida miaka miwili baadaye.

Ribadu ndiye mgombea kijana kabisa akiwa amezaliwa mwaka 1960, na ndiye aliyekuwa mkuu wa kamisheni ya kupambana na ufisadi nchini Nigeria, ambayo ilichukua hatua kali dhidi ya mafisadi nchini humo kati ya mwaka 2005 na 2006.

Uchaguzi wa leo unatarajiwa kurejea mafanikio ya uchaguzi wa bunge wa wiki iliyopita, ambao pamoja na matukio ya hapa na pale, umetajwa kuwa ulikuwa mzuri zaidi kulinganisha na chaguzi zilizopita nchini humo.

0 comments:

Post a Comment