SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 6, 2011

MAELFU WACHANGAMKIA KIKOMBE CHA 'DADA' TABORA

Margareth Mutalemwa akiomba kabla ya kumpatia kikombe mmoja wa wagonjwa waliofika kwake eneo la Uzunguni Manispaa ya Tabora kupata dawa.
Na Juma Kapipi, Tabora
TANGU kujitokeza kwa mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Margareth Mutalemwa (40), mkazi wa eneo la Uzunguni hapa Manispaa ya Tabora ambaye amedai kuwa ameoteshwa njozi iliyomuelekeza kutoa tiba ya magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi, maelfu ya watu wamekuwa wakichangamkia tiba hiyo mbadala inayotolewa kwa kikombe kwa gharama ya shilingi mia tano.
Ingawa hali hiyo ya kujitokeza kwa mwanamke huyo imeonekana kama ni mbinu ambayo ameiiga kutoka kwa Mchungaji Ambilikile Masapile wa Loliondo, mwanamke huyo anaendelea kujichukulia umaarufu kwa kile kinachoonekana hasa kutoa tiba hiyo kwa baadhi ya wagonjwa wanaoonekana kuwa wanapata unafuu kwa muda mfupi wakiwemo viongozi mbalimbali na watu maarufu.
Licha ya kuwepo kwa mafanikio yanayoelezwa zaidi na watu waliopatiwa tiba hiyo, baadhi ya viongozi wa kidini wamekuwa wakipingana na mama huyo na hata baadhi yao wakidai kuwa amekumbwa na mapepo yanayompotosha ili kuwatoa watu kwenye mlengo wa dini zao.
Aidha kuna taarifa kuwa mama huyo ambaye ni muumini wa dini ya Kikristo madhehebu ya Roman Catholic, aliitwa katika moja ya makanisa yaliyopo mjini hapa kumtaka athibitishe ukweli wa tiba yake na yeye kufanya hivyo.
Tukio la mama huyo lilipiga hodi pia kwa Baba Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Mhashamu Paul Ruzoka na hivyo kutakiwa kulitolea ufafanuzi kuhuLinksu msimamo wa kanisa ambapo alisema kanisa halitakuwa na pingamizi ikiwa mama huyo tiba anayoitoa atakuwa anamtaja Mwenyezi Mungu, akaongeza pia kuwa kanisa linahitaji muda zaidi wa kupata ushuhuda wa tiba hiyo ambayo kwa sasa inakubaliwa na wengi.
Sambamba na tiba hiyo ya maji ya dawa ya mitishamba ambayo serikali imeamua kuchukua sampuli kwa lengo la kuifanyia uchunguzi kuangalia kama ina madhara kwa binadamu, idadi kubwa ya watu hasa kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wamekuwa wakiendelea kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya kikombe hatua ambayo imesababisha kuwepo kwa misururu ya umati mkubwa wa watu wanaokesha katika foleni bila kujali mvua wala jua kali.
Kufuatia hali hiyo serikali pia imeamua kuboresha miundo mbinu ya barabara ya kwenda nyumbani kwa mama huyo ambayo kwa sehemu kubwa ilikuwa imeathiriwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sasa.
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO:BOFYA

0 comments:

Post a Comment