SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 6, 2011

IPTL YATAFUNA BILIONI 15 KWA MWEZI

Waziri wa Nishati na Madini Mhe.William Ngeleja.
Na.Mwandishi wetu,Dodoma
Wastani wa Bilioni 15.62 hutumika kwa kila mwezi kwa ajili ya kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL ili kuzalisha umeme nchini.
Akijibu swali bungeni leo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa tani zaidi ya 12,000 za mafuta mazito kwa mwezi. “Kiasi cha Sh bilioni 46.4 au wastani wa shilingi bilioni 15.62 kwa kila mwezi zinalihitajika kwa kugharamia ununuzi wa tani 36,800 za mafuta mazito (HFO) kwa kipindi cha miezi mitatu.”Alisema. Alisema matumizi hayo yalitumika kuanzia Novemba 15, 2010 hadi Februari 14, 2011 ambayo ni sawa na tani 400 kwa siku. Alisema Kampuni ambazo serikali imekuqwa ikinunua mafuta hayo kutoka kwao ni Oryx na Total kwa kuwa ndizo kampuni pekee zinazofanya biashara ya mafuta mazito nchini. Alisema utaratibu uliotumika kupata kampuni za Oryx na Total ni kwa njia ya “Restricted Tendering” ambapo kampuni za mafuta zilitakiwa kufikisha mafuta maghala ya IPTL mwezi Novemba 2010. “Katika hali ngumu kama hiyo maamuzi ya serikali yalihitajika kufanyika haraka ili kupunguza ukali wa mgawo wa umeme kwenye mfumo wa gridi ya Taifa,” alisema Ngeleja. Alisema fedha za kununua mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo zimetoka kwenye mfuko mkuu wa Serikali. Aidha alisema mpango wa kubadilisha mitambo ya IPTL ili iwezeLink kutumia gesi asilia badala ya mafuta alisema serikali haiwezi kufanyika kwa sasa kutoakana na kuwepo kwa kesi mahakamani. Alisema mara baada ya kumalika kwa kesi hiyo mahakamani serikali itafanya hivyo ili kuweza kupunguza gharama za uendeshaji. Alikuwa akijibu swali la Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini Chadema) aliyetaka kujua kiasi cha mafuta kinachonunuliwa kila mwezi kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya IPTL.
CHANZO

0 comments:

Post a Comment