SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, March 25, 2011

DARAJA LA KIGAMBONI KUGHARIMU BILIONI 130

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli( wa pili kutoka kushoto) akiangalia mchoro wa Daraja la Kigamboni linalotarajia kujengwa kwa ushirikiano baina ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na Wizara ya Ujenzi. Mchoro huo ulionyeshwa jijini Dar es salaam na Ofisa Mwandamizi wa Miradi wa NSSF Engineer John Ndazi (wa pili kutoka kulia). NSSF inatarajia kuanza ujenzi wa Daraja hilo mapema mwaka huu na litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 130 hadi litakapokamilika.
Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli (wa tatu kutoka kushoto) akipata maelez katika eneo la Kurasini Vijibweni jijini Dar es salaam kutoka kwa Meneja Miradi wa NSSF Engineer John Msemo (kulia) juu ya eneo ambalo watajenga Daraja la Kigamboni. Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii linatarajia kuanza ujenzi wa Daraja hilo mapema mwaka huu mara baada ya zabuni kutangazwa na kumpata mhandisi.Daraja hilo litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 130 hadi litakapokamilika.
Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli( kushoto) akisisitiza umuhimu wa uharikishaji wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni ili kurahisisha usafiri baina ya Kigamboni na maeneo ya mjini. Magufuli alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam wakati akikagua eneo ambalo Daraja hilo linatarajiwa kujengwa na NSSF kwa ushirikiano na Wizara ya Ujenzi na litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 130 hadi litakapokamilika.
(Picha na Tiganya Vincent-Habari Maelezo- Dar es salaam).

0 comments:

Post a Comment