Polisi ya Uingereza yakandamiza maandamano ya Wanachuo
Polisi ya Uingereza imepambana na makumi ya maelfu ya wanachuo mjini London wanaolalamikia mpango wa kuongezwa ada za Vyuo Vikuu. Hatua ya polisi kuingilia kati maandamano hayo kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji hao ilipelekea kutokea vurugu na mapigano baina yao na wanachuo hao.
Wanachuo hao waliandamana na kwenda kusimama mbele ya jengo la Bunge la Uingereza, maandamanao ambayo yamekwenda sambamba na kuanza kikao cha Bunge kinachojadili mpango wa kuongeza ada za Vyuo Vikuu.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, mpango wa kuongezwa ada za Vyuo Vikuu nchini Uingereza umepasishwa katika bunge la nchi hiyo licha ya upinzani mkali wa wanachuo.
Kwa utaratibu huo kuanza sasa ada ya Vyuo Vikuu vya Uingereza itakuwa pauni 9,000 kwa mwaka badala ya pauni 3,290, ongezeko ambao linalalamikiwa mno na wanachuo pamoja na jumuiya mbalimbali za wanachuo nchini humo
0 comments:
Post a Comment