SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, November 11, 2010

Tanzania Yang'ara Kwenye Maonesho Ya WTM London
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Nzuki (kuume) akiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hio Bw. Geoffrey wakijadiliana jambo kwenye banda letu
Katika maonyesho ya Dunia ya Masoko ya Usafiri na Utalii (WTM) London mwaka huu,Tanzania imeanda hafla ya pamoja na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hafla hii ili wajumuisha Waziri wa utalii toka uganda, Naibu Katibu Mkuu wa Afrika Mashariki, Mabalozi wa Tanzania,Rwanda, Uganda na Kenya.
Vilevile walikuwepo wawakilishi wa kiserikali na makampuni binafsi yafanyayo biashara za mbugani na utalii. Maonyesho haya ambayo hufanyika kila mwaka, hujumuisha nchi mbalimbali duniani ambazo hukusanyioka na kujaribu kujiuza na kujitangaza.
Kwa serikali na makampuni ya Kitanzania yafanyayo biashara hii huu ni mwaka wao wa kumi na moja katika kujishirikisha na maonyesho haya. Na kwa ukweli ulio wazi, banda la Tanzania limeng'ara sana, hongera kwa walio li-design kwani wamefaya kazi nzuri na ya kuvutia watalii
Balozi wetu Uningereza Mh. Peter Kallaghe (wa pili kuume) akiwa na mabalozi wa nchi za Afrika Mashariki walioalikwa kwende hafla iliyofanyika banda la Tanzania
Msanii Diamond alikuwepo kutumbuiza
Mkuu wa kitengo cha biashara katika ubalozi wetu
Uingereza Bw. Y. Kashangwa akifurahia fanaka ya hafla hii
Vijana wa Urban Pulse wakiwa na
Balozi Kallaghe na Dr Weggoro baada ya hafla

0 comments:

Post a Comment