SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, November 10, 2010

BREAKING NEWS: USIPIKA! MWANAMKE KUWA SPIKA!
Anna Makinda
Anna Abdallah
Kate Kamba
Habari zilizotua hivi punde kutoka DODOMA zinasema kuwa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, imependekeza majina matatu ya wanachama wake kuwania kiti cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na Channel Ten usiku huu katika taarifa yake ya habari ya saa moja, wanachama hao waliopitishwa ni Anna Abdallah, Anna Makinda na Kate Kamba (pichani). Hii ina maana kwamba, Mh. Samuel Sitta, aliyekuwa akitetea kiti chake na Andrew Chenge na wengine, wote majina yao yamekatawaliwa! vile Vile hii ina maana kwamba, kwa mara ya kwanza, Spika wa Bunge anatarajiwa kuwa mwanamke!!
chanzo:  http://www.globalpublishers.info

0 comments:

Post a Comment