Afisa wa zamani wa ngazi za juu katika jeshi la Uganda amekwenda mahakamani kupinga azma ya Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo ya kutetea wadhifa wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Maguru Ruhinda ameitaka mahakama kuu ya Uganda kubatilisha uteuzi wa Museveni kuwa mgombea urais kwa tikiti ya chama tawala cha NRM kwa madai kuwa chama hicho kilimzuia asimpinge Rais Museveni kwenye uchaguzi wa chama mwezi uliopita. Ruhinda pia ameitaka mahakama imchukulie hatua za kisheria katibu mkuu wa NRM Amama Mbabazi kwa kumzuia kugombea uongozi wa chama hicho. Rais Museveni ambaye amekua uongozini tangu mwaka 1986 anatetea wadhifa wake huku akiwa Rais aliyetawala kwa muda mrefu zaidi katika eneo la Afrika Mashariki.
Wednesday, September 22, 2010
Azma ya Rais Museveni ya kutetea wadhifa wake mwaka ujao yapingwa kortini
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Wednesday, September 22, 2010
Email This
BlogThis!
Share to Twitter
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment