SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, August 25, 2010

NDOTO ZA UTURUKI ZAFIKIA MWISHO
Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Brazil Róbson de Souza Robinho amefuta ndoto zake za kujiunga na klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki na badala yake anataka kujiunga na moja ya klabu za nchini Italia ama Hispania.
Róbson de Souza Robinho ametoa msimamo huo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini kuahidi kulifanyia kazi suala la mchezaji huyo anaetaka kuondona City Of Manchester.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema alitamani sana kuelekea nchini Uturuki baada ya uongozi wa klabu ya Fenerbahce kutuma ofa ya kutaka kumsajili lakini, ameonea ni bora arejee Hispania ama kuelekea nchini Italia.
Hata hivyo bado kuna shaka juu ya usajili wa mchezaji huyo kwa kuhofia huenda akashindwa kuuwahi muda wa usajili unaofikia kikomo August 31 mwaka huu.

*********************
UKAME SASA BASI

Kiungo wa kimataifa toka nchini Urusi na klabu ya Arsenal Andrey Arshavin amesema baada ya The Gunners kumaliza misimu mitano bila kutwaa ubingwa wa michuano yoyote, wakati umewadia kwa klabu hiyo kufanya vyema.
Akitoa sababu za kuipa nafasi Arsenal msimu huu Andrey Arshavin amesema anaamini kikosi chao msimu huu kimepevuka kwa kiwango kikubwa hivyo ni jambo gumu sana kwao kumaliza pasipokua na ubingwa wa ligi.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 ameongeza kuwa msimu uliopita walikaribia kufanya vizuri tena kwa kuzipa mshawasha klabu ya Chelsea pamoja na Man Utd na mwisho wa ligi walijikuta wakizidiwa point chache na klabu hizo ziliomaliza katika nafasi mbili za juu.

0 comments:

Post a Comment