Uchunguzi mpya
wa maoni uliofanywa na gazeti mashuhuri la The Washington Post kwa
ushirikiano na kanali ya televisheni ya ABC nchini Marekani umeonyesha
kuwa umaarufu wa Rais Barack Obama wa nchi hiyo umepungua kwa kiwango
kikubwa. Matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kuwa takriban asilimia 60
ya Wamarekani hawana imani na Rais Obama hususan katika upande wa
kufanya maamuzi muhimu yanayoiathiri nchi yao. Weledi wa masuala ya
kisiasa wamesema kuwa kushindwa stratejia za Washington huko Afghanistan
na Iraq na suala la kuvuja mafuta ya petroli katika ghuba ya Mexico
ambapo Marekani hadi sasa haijafanikiwa kulitatua tatizo hilo ni
miongoni mwa mambo yaliyopelekea kiongozi huyo apoteze zaidi umaarufu
wake. Mwaka mmoja uliopita Rais Obama alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri zaidi duniani lakini hali hiyo imekua ikibadilika kila uchao.
*******************
Mwakwere ahifadhi kiti chake cha ubunge kwenye uchaguzi
mdogo wa Matuga nchini Kenya |
|
|
|
Ali Chirau
Mwakwere amefanikiwa kukihifadhi kiti chake cha ubunge kwenye uchaguzi
mdogo wa eneo bunge la Matuga. Mwakwere ambaye anatoka katika chama cha
PNU kinachoongozwa na Rais Mwai Kibaki, amepata kura 16,350 na hivyo
kumshinda mpinzani wake wa karibu Hassan Mwanyoha kutoka chama cha ODM
kinachoongozwa na Waziri Mkuu Raila Odinga aliyepata kura 10,887. Ali
Chirau Mwakwere Waziri wa zamani wa Uchukuzi alivuliwa ubunge na
mahakama moja ya Mombasa kufuatia kesi iliyokuwa imewasilishwa
mahakamani kupinga kuchaguliwa kwake wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka
2007 kwa madai kuwa aliiba kura kwenye uchaguzi huo. Nafasi ya Uwaziri
aliyokuwa akishikilia hadi alipovuliwa ubunge hadi sasa haijapewa mtu
mwengine na inatarajiwa kuwa atarejeshewa wadhifa huo na Rais Kibaki
baada ya kuapishwa upya bungeni.
|
| | | | |
0 comments:
Post a Comment