Takriban watu 23 wameuawa katika milipuko miwili
iliotokea kwenye mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Haijajulikana mpaka sasa milipuko hiyo
imesababishwa na nini, ambapo polisi wamesema imelipuka katika klabu ya
mchezo wa raga na kwenye mgahawa, wakati mashabiki walipokuwa wakitazama
Kombe la Dunia.
Inspekta wa Polisi Kal Kayihura ameliambia
shirika la habari la AFP, “ Kwa hakika mabomu haya yalikuwa yakilenga
watu waliokusanyika kuangalia Kombe la Dunia.”
Wanamgambo wa Kisomali hapo awali waliwahi
kutishia kushambulia mji wa Kampala; majeshi ya Uganda yapo mjini
Mogadishu kulinda amani.
Bw Kayihura ameliambia shirika la habari la AP
kwamba anaamini kundi la wanamgambo la al-Shabab linahusika na shambulio
hilo.
Baada ya tukio moja miongoni mwa milipuko hiyo
Bw Kayihura alisema, “ Taarifa tulizonazo zinaonyesha kwamba watu 13
wamekufa hapa katika mgahawa wa Ethiopian village na wengine wengi
wamejeruhiwa na zaidi ya 10 wameripotiwa kufariki dunia katika klabu ya
raga.”
Takriban majeshi 5,000 ya Afrika ya kutunza
amani kutoka Uganda na Burundi yapo kwenye mji mkuu wa Somalia,
Mogadishu kuilinda serikali ya mpito iliyopo.
Jeshi hilo la Amisom limejikuta kwenye mapigano
na wanamgambo wanaodhibiti eneo kubwa la Somalia ya kati na kusini. bbc swahili
0 comments:
Post a Comment