Hakuna mpasuko wa uhusiano kati yetu;Obama, Netanyahu
Rais wa Marekani, Barack Obama amesema anatarajia mazungumzo ya ana kwa ana mashariki ya kati kuanza kabla ya mwisho wa mwezi Septemba, huku kiongozi huyo na waziri wa Israel, Benjamin Netanyahu wakikanusha madai kwamba kuna mpasuko katika uhusiano wao.
Viongozi hao waliketi
karibu na walisalimiana kwa muda mbele za kamera wakinuia kusitisha
wasiwasi uliojiri katika mkutano wao wa faragha wa mwezi machi katika
ikulu ya Marekani
Rais wa Marekani,
Barack Obama amesema anaamini kwamba waziri mkuu wa Israel, Benjamin
Netanyahu anataka amani na kwamba anaamini yuko tayari kuchukua hatua
mahsusi kwa ajili ya amani. Rais Obama aliyasema hayo huku akilipinga
suala lililoashiria kwamba alikuwa ameitenganisha Marekani kutoka kwa
Israel.
Bw Obama alisema
kilicho wazi ni kwamba amekuwa akimuamini waziri mkuu Netanyahu tangu
akutane naye kabla ya kuchaguliwa raia na kwamba amekiri hivyo hadharani
na faraghani.
Mazungumzo hayo
yalifanyika wakati kukiwa hali ya wasiwasi kuhusiana na na kusitishwa
kwa muda, ujenzi wa makaazi kwa walowezi wa kiyahudi na muda huo
unakamilika mwishoni mwa mwezi Septemba.
Rais Obama akiligusia
suala hilo alisema anatarajia mchakato wa mazungumzo ya ana kwa ana
kutoka kwa ule wa upatanishi unaoongozwa na Marekani kati ya Wa-Israeli
na Wapalestina, yataufanya muda huo wa mwisho usiwe na maana.
Bw Netanyahu amesema
yuko tayari kukutana na kiongozi wa mamlaka ya ndani wa Palestina,
Mahmoud Abbas wakati wowote lakini Wapalestina bado hawajajitolea kwa
mazungumzo ya ana kwa ana huku wakiituhumu Israel kwa kudharau mazingira
hayo kwa kuendeleza juhudi za ujenzi wa makaazi. Bw Netanyahu alisema
walijadiliana kuhusu mkakati muafaka utakaofuatwa sasa.
Changamoto kwa sasa ni
kuwashawishi Wapalestina kukubali muda wa utekelezaji ambao rais Barack
Obama anao akilini. Kulingana na Nabil Abu Rudeina, msemaji wa Rais wa
Mamlaka ya ndani wa Palestina, Mahmoud Abbas, kionmgozi huyo anasisitiza
juu ya umuhimu wa mazungumzo ya upatanishi kuhusu masuala tete ya
mipaka na usalama, kabla ya kuingia katika mazungumzo ya ana kwa ana.
Waziri mkuu wa Israel
anashinikizwa na chama chake cha mrengo wa kulia kwamba asiyafuate
matakwa ya Marekani ya kusogeza mbele muda wa kusitisha ujenzi.
Bw Netanyahu anakutana
leo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa , Ban Ki moon na ameonya kwamba
kitisho kwa Israel ni mpango wa nyuklia wa Iran na aliupigia upatu
juhudi ya Marekani ya kuiwekea vikwazo Iran.
Mwandishi, Peter Moss
0 comments:
Post a Comment