SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, July 3, 2010

Gari la mafuta laangamiza 220 Kongo
Zaidi ya watu 220 wanahofiwa kufa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Watu hao wameangamia baada ya lori moja lilobeba mafuta kuanguka na kuwaka moto katika kijiji cha Sange, mashariki mwa nchi hiyo.
Inaarifiwa kuwa watu hao walikuwa wakijaribu kuchota mafuta kutoka lori hilo, lilokuwa limepinduka, baada ya dereva wake kushindwa kulidhibiti.
Afisa huyo amesema lori hilo lilipinduka kutokana na ajali ya barabarani, na kulipuka kwa lori hilo kulisababishwa na kuvuja kwa mafuta. Umoja wa Mataifa umesema walinzi wa amani watano wa umoja huo waliokuwa wakilinda utaratibu kwenye sehemu iliyotokea mlipuko huo waliuawa.
Ujumbe  wa  Umoja  wa  Mataifa  unaripoti  kuwa  watano kati  ya  wanajeshi  wake  wa  kulinda  amani  pia wameuwawa  wakati  wakijaribu  kuwazuwia  watu kukaribia  lori  hilo.
Lori  hilo  lilikuwa  linasafirisha  mafuta   kutoka  katika  nchi jirani  ya  Tanzania   na  lilipinduka  kutokana  na mwendo wa  kasi , katika  kijiji  cha  Sange, kiasi  cha  kilometa  30 kaskazini  ya  mji  wa  Uvira  karibu  na  mpaka  na Burundi.
Wakati  huo  huo  watu  13  wameuwawa  na  wengine wanane  wamejeruhiwa  kwa  kuungua  vibaya  kaskazini mwa  Nigeria  wakati  lori  la  kusafirisha  mafuta lilipopinduka  na  kuripuka   jana  Ijumaa , katika  kijiji  cha Gombe.

0 comments:

Post a Comment