Hongera
kwa Wagombea
Mama Salma Kikwete akimpongeza mai hazbendi wake
Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa kwa zaidi
ya asilimia 99 kuwa mgombea pekee wa Urais kwa tiketi ya CCM usiku wa
kuamkia leo ukumbi wa Kizota mjini DodomaMwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein(kushoto) na mgombea mwenza bara Dr.Mohamed Gharib Bilal kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCMMwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pampja na Rais wa Zanzibar Amani Abedi Karume(kulia) pamoja na Makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein(wapili kushoto), pampja na mgombea mwenza Dr.Mohamed Gharib Bilal mwishoni mwa mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Picha na Freddy Maro
****************************
Dakta Gharib Bilal ateuliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais Jakaya Kikwete JK AKIMPONGEZA DK. GHALIB BILAL
Dakta Gharib Bilal ateuliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais Jakaya Kikwete JK AKIMPONGEZA DK. GHALIB BILAL
DK. GHALIB BILALI AKIPONGEZWA NA MZEE KINGUNGE NGOMBALE
MWIRU. KATI NI MH. FREDERICK SUMAYE
Dokta Gharib
Bilal aliyekuwa mgombea wa kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya CCM
katika uchaguzi wa urais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi mstaafu,
ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi
mkuu ujao. Kwa utaratibu huo Dakta Bilal atakuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo CCM itaibuka na ushindi katika
uchaguzi ujao wa Oktoba 31. Kabla ya kutamkwa kwa jina la Dk. Bilal jana
saa tatu usiku, kura za ndiyo zilipigwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
CCM, uliokuwa ukifanyika mjini Dodoma kumthibitisha Kikwete kupeperusha
bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Akitangaza
matokeo ya kura hizo jana jioni, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais
Amani Abeid Karume, alisema asilimia 99.16 ya wajumbe walipiga kura za
Ndiyo kumthibitisha Rais Kikwete kuwa mgombea wa urais wa CCM katika
uchaguzi mkuu ujao.
0 comments:
Post a Comment