Chama cha CCM kuteua Wagombea wa Urais
Wajumbe wa chama tawala nchini
Tanzania, Chama cha Mapinduzi, CCM, wanakutana leo mjini Dodoma,
kuwateua wagombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania pamoja na
wagombea wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Kumekuwa na kampeini za usiku kucha huku
wagombea wakiwashawishi wajumbe kuwaunga mkono.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini
humo, watu watano wamejitokeza kuwania kiti cha Urais kisiwani
Zanzibar.
Watano hao ni pamoja na waziri wa zamani Dr
Mohamed Bilal, makamu wa rais Dr Ali Mohamed Shein, waziri kiongozi
Shamsi Vuai Nahodha, na naibu wake Ali Juma Shamhuna na waziri wa elimu
Amali Haroun Ali Suleiman.
Watano hao watakuwa wakiwania nafasi ya
kumrithi rais Amani Karume ambaye muda wake wa kuhudumu kama rais
unamalizika mwaka huu.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano Jakaya Kikwete,
anatarajiwa kuidhinishwa tena kuwania kiti hicho kwa muhula wa pili.
Kufikia sasa hakuna mwanasiasa yeyote ambaye
amejitokeza kumpinga rais Kikwete. Matokeo ya kongamano hilo
yanatarajiwa kutolewa baadaye hii leo. bbc swahili.
0 comments:
Post a Comment