SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, June 10, 2010

Vikwazo vya UN ni upuzi mtupu, Iran


Waandamanaji nchini Iran
   Iran imepuuzilia mbali vikwazo vilivyowekewa nchi hiyo na baraza la usalama la Umoja wa mataifa kwa sababu ya mpango wake wa nuklia.
   Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinajad ametaja vikwazo hivyo kama uzembe usio na maana yoyote na kusema kuwa thamani yake ni tambara bovu lililotumika.
   Vikwazo hivyo vipya vinaipiga marufuku Iran kununua silaha nzito na kuweka sheria ngumu zaidi za kufanya biashara na mabenki nchini humo.
   Pia vimeongeza idadi ya viongozi wa nchi hiyo waliopigwa marufuku kusafiri nje. Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa vikwazo hivyo ni hafifu kuliko ilivyotarajiwa na mataifa ya magharibi kutokana na shinikizo la Urusi na China. BBC SWAHILI
             **********************
Watu 39 wauawa katika mlipuko uliotokea harusini nchini Afghanistan

Sample ImageWatu wasipungua 39 wameuawa na 73 wengine kujeruhiwa baada ya kutokea mripuko katika sherehe za harusi katika mkoa wa Kandahar wa kusini mwa Afghanisan.
Wengi wa waliouawa na kujeruhiwa katika mripuko huo ni wanawake. Mripuko huo umetokea wakati hadhirina walipokuwa wanakula chakula cha dhifa hiyo katika wilaya ya Arghanab iliyoko umbali wa karibu kilomita 30 kutoka mji wa Kandahar.
Watoto wadogo 10 ni miongoni mwa waliojeruhiwa katika mripuko huo.
Hadi tunapokea habari hii ilikuwa haijajulikana mripuko huo umesababishwa na kitu gani.
Afisa mmoja wa hospitali kuu ya Kandahar amewaambia waandishi wa habari kuwa bado hawajajua ni watu wangapi hasa wameuawa na vile vile hawajui mripuko huo ulikuwa ni wa kujitoa muhanga, wa bomu au wa kitu gani kingine.
Idadi ya wahanga wa mripuko huo ni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika tukio moja kwa miezi kadhaa sasa nchini Afghanistan. KISWAHILI RADIO.IRIB.IR

0 comments:

Post a Comment