SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, June 10, 2010

RICHIE ONE HATIMAE ATANGAZA KUNDI JIPYA CHINI YA KAMPUNI YA MPO AFRICA

Hatimae Kampuni ya Mpo Afrika imetangaza kusaini mkataba na kundi jipya litakalokuwa likiitwa Wanaume, likiundwa na wanamuziki walioachwa katika kundi la TMK Wanaume Halisi.
   Akizungumza msemaji wa kundi hilo mapema leo ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,Hassan Umande alisema lengo la kuunda kundi hilo jipya ni kwa ajili ya kuendeleza sanaa na kuleta mabadiliko katika anga ya muziki wa kizazi kipya aka bongofleva hapa nchini.
   "Mnajua waandishi, kiukweli kuna vikwazo vingi vilitokea mpaka tukaamua kujitenga ,yote hiyo kuepuka migongano ambayo kimsingi si ya lazima kwa sababu sisi wote ni vijana na tunatafuta maisha,kwa hiyo kwa sababu tumetengwa basi tumeamua kuunda kundi la watu sita"'amebainisha Hassani Umande.
   Hassani amewataja wasanii watakaounda kundi hilo kuwa ni Athuman Yahya (A.Man), Juma Mbelwa (Juma Jazz), Karim Kaiman (Kakaman), Abdul Ally (Mzimu), Richard Shauri (Rich One) pamoja na David Mpangile (Daz-p).
Alisema mpaka sasa wamesharekodi nyimbo tatu ikiwemo, mapenzi kitu gani?, Poa tu pamoja na Mukide 
Muda Wowote Kuanzia Sasa Watatoa Single Yao Mpya Itakayotambulisha Kundi Hili.
                     *********************************
MSANII MPYA SAJNA ANAKUJA
   Habari mpya kuhusu SAJNA ni kwamba, kwa sasa yupo jijini Dar kwa lengo la kujitangaza zaidi na pia kuitangaza album yake ya 1 ambayo iko katika hatua za mwisho kukamilika na itakuwa sokoni mwezi 1 kuanzia sasa..
   Album inaitwa IVETA, itakuwa na jumla ya nyimbo 10, baadhi ni IVETA, BINADAMU, MBALAMWEZI, SUBIRA, MGANGA, ROHO MBAYA, NADHIFA nk.
Katika album hii atawashirikisha BELLE 9, LINAH na JOSEFLY.. Lengo la kuwashirikisha wasanii wachache ni kutaka kukionesha kipaji chake zaidi..
   Studio zilizohusika kuipika album hii ni pamoja na TETEMESHA RECORDZ (Kid bwoy), AB RECORDS (Amba), MUSIC LAB (Duke), MZUKA RECORDS (Benja), A2P RECORDS (Sam Timba)
Tafadhali tuipokee album yake itakapoingia sokoni.

0 comments:

Post a Comment