Madaktari wa vyeo vya chini
nchini Nigeria, wameanza mgomo wa siku tatu, kulalamikia mishahara ndogo
wanayopata na hali duni ya utendaji kazi.
Madaktari hao wanadai kuwa mafunzo yanayotolewa
na taasisi za matibabu nchini humo ni ya chini zaidi na kwamba serikali
ya nchi hiyo haina nia ya kutatua tatizo hilo.
Chama cha madaktari nchini Nigeria,
kinawakilisha madaktari wa vyeo vya juu pekee na kimetangaza kuwa
hakitashiriki kwenye mgomo huo.
Juhudi hizi zinafanyika huku uchaguzi mkuu nchini humo ukitarajiwa mapema mwaka ujao.
Rais wa sasa wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza kuwa atamteua mkuu mpya wa tume ya uchaguzi baadaye wiki hii, ingawa wanharakati wa demokrasia wanapinga rais kuwa na mamlaka ya kumteua mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi.
BBC Swahili
Raia kutoa maoni kuhusu katiba:Nigeria
Wabunge wa Nigeria leo wataanza
kupokea maoni na mapendekezo ya umma kuhusu mabadiliko ya katiba kama
juhudi zao za kutaka kurekebisha katiba ya nchi.
Wale watakaotaka kutoa maoani yao, watakusanyika
katika majengo ya bunge mjini Abuja. Kumekuwepo na madai kuwa uchaguzi
wa mwaka 2007 na ule wa 2003 ulikumbwa na wizi wa kura na udanganyifu.Juhudi hizi zinafanyika huku uchaguzi mkuu nchini humo ukitarajiwa mapema mwaka ujao.
Rais wa sasa wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza kuwa atamteua mkuu mpya wa tume ya uchaguzi baadaye wiki hii, ingawa wanharakati wa demokrasia wanapinga rais kuwa na mamlaka ya kumteua mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi.
BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment