Wanawake watatu Namibia
wanaishtaki serikali kwa madai ya kuhasiwa bila idhini yao baada ya
kupimwa na kuonekana na virusi vya ukimwi.
Wanawake hao wanasema madaktari na wauguzi
walitakiwa kuwaelea uzuri kitu gani kilikuwa kikiendelea.
Shirika la utetezi linalowawakilisha, the Legal
Assistance Centre LAC, limesema limekusanya ushahidi kutoka kesi 15 za
madai ya kuhusika na kuhasiwa baada ya kuonekana na virusi vya HIV
katika hospitali tangu mwaka 2008.
Maandamano ya kuwaunga mkono wanawake hao
inaendelea huko Windhoek huku kesi ikianza.
Mwandishi wa BBC Frauke Jensen aliyopo kwenye
mji mkuu huo, amesema kuna takriban waandamanaji 300.
Wengi wao ni wanawake, wakiwa na kauli mbiu yao "
Mwili wangu, fuko langu la uzazi, haki yangu," na wakishika mabango
yakisema: " Kwanini umenihasi?"
Pia wana mpango wa kufanya maandamano mengine
siku ya Jumatano katika hospitali mbili ambapo inadaiwa shughuli hizo za
kuhasi zilipofanyika.
"Usawa kwa wote"
Wanawake hao wanaofikisha kesi zao mahakamani
wanataka dola za kimarekani 130,000 kama fidia kutoka wizara ya afya.
Msemaji wa wizara hiyo, Gladys Kamboo, amesema
hawezi kuzungumzia lolote kuhusu kesi hiyo wakati tayari imefikishwa
mahakamani, lakini amesisitiza kuwa wizara hiyo haijawadhuru wanawake
hao kwa makusudi.
Shirika la LAC limesema mahakama kuu imetaka
wanawake hao wasijulikane ili kuzuia " ubaguzi na unyanyapaa zaidi
kutokana na hali yao ya kuwa na virusi vya HIV."
Amon Ngavetene wa LAC ameiambia BBC, " Tunataka
mfumo wa afya ulio kwenye misingi ya haki za binadamu na unaotoa haki
kwa wote."
Amesema wakati wanawake wenye virusi vya HIV
wanapokwenda hospitali, mara nyingine hushauriwa kuhasiwa kwa siri na
madakatari wao.
Bw Ngavetene amesema wanawake hawa si mara zote
hupewa maelezo ya nini hasa hufanyika na hatari inayowakabili si
aghalabu kushughulikiwa.
Pia amesema huenda kukawa na tatizo la lugha
hasa katika nchi hiyo yenye lugha za asili 11.
Mbali na maandmano hayo huko Windhoek, mengine
yanatarjiwa kufanyika siku ya Jumanne huko Afrika Kusini, Zambia,
Uingereza na Marekani. BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment