Kiongozi wa vijana katika chama
tawala cha African National Congress ANC, nchini Afrika Kusini ametetea
mienendo yake baada ya kuadhibiwa na chama chake.
Katika mahojiano ya kipekee na BBC, Malema amekataa kukubali kuwa alitenda makosa na kusema kwamba anahisi kutelekezwa na watu ambao alikuwa akiwategemea ndani ya chama hicho.
Amesema uchumi wa taifa hilo umegawanyika kwa misingi ya kikabila na kwamba ataendelea kupigania haki za Waafrika weusi ambao wamekandamizwa.
Malema ameongeza kusema kuwa huenda asikome kuimba wimbo ulioimbwa wakati wa harakati za ukombozi wa taifa hilo ambao una maneno yanayosema ''ua wazungu''. Mahakama moja nchini Afrika Kusini ilimzuia Malema kuimba wimbo huo hadharani.
BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment