Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amekiri kuwa mazungumzo ya mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel yamegonga mwamba. Abbas ameashiria kuanza kwa duru mpya ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana ya mapatano kati ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala wa Kizayuni na kusema kuwa kutokana na ukorofi na pingamizi za upande wa wazayuni hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana hadi sasa katika mazungumzo hayo. Kuhusiana na mpango wa kubadilishana ardhi na Wazayuni, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema Mamlaka hiyo iko tayari juu ya suala hilo lakini bado kuna hitilafu juu ya ukubwa wa ardhi hizo. Mahmoud Abbas ametangaza uungaji mkono wake juu ya mpango wa kubadilishana ardhi na utawala wa Kizayuni katika hali ambayo Saeeb Uraiqat, afisa mwandamizi wa timu ya mazungumzo ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina amekanusha uvumi uliopo juu ya suala hilo na kusema kwamba utoaji wa habari za aina hiyo si uwajibikaji.
Kiswahili Radio. |
0 comments:
Post a Comment