MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu, leo imesoma Hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi
wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus
Liyumba,Katika hukumu hiyo Liyumba amepatikana na hatia na kuhukumiwa
kwenda jela miaka miwili dhidi ya kesi ya utumiaji mmbaya wa madaraka .
Awali Liyumba alifikishwa mahakamani hapo
akiwa pamoja na aliyekuwa meneja miradi wa BoT Deogratius Kweka, ambapo
kwa pamoja walikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutumia vibaya
madaraka aliyokuwa nayo, jambo lililopelekea serikali kupata hasala ya
sh bilioni 221, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.
Hata
hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa
mashtaka, upande wa mashtaka ulimuachia aliyekuwa mshtakiwa mwenza wa
Liyumba {Kweka}, na kumshitaki Liyumba kwa kesi hiyo.Upande huo wa
mashtaka uliita mahakamani hapo mashahidi 8, wakiwamo waliokuwa wajumbe
wa bodi ya wakurugenzi wa BoT, pamoja na kutoa vielelezo mbali mbali
vinavyohusiana na kesi hiyo.
Baada ya
ushahidi huo kumalika kusikilizwa, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumfutia
Liyumba shtaka la kuisababishia serikali hasala ya bilioni 221 baada ya
Upande huo wa serikali kupitia ushahidi na vielelezo vyake kushindwa
kuithibitishia mahakama hiyo kama Liyumba alihusika na kosa
hilo.Kufuatia uamuzi huo, mahakama ilimtaka Liyumba kujitetea juu ya
uhusika wake katika shtaka la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.
Katika
utetezi wake Liyumba alijitetea mwenyewe kama shahidi wa kwanza kutoka
upande wa utetezi, na baadae alimwiita shahidi wa pili ambaye ni Bosco
Ndimbo Kimela, aliyekuwa katibu wa BoT.Baada ya kumaliza usikilizwaji wa
ushahidi huo, mahakam hiyo ilizitaka pande zote mbili kuwasilisha hoja
zao za kisheria, ambapo alipanga kusoma hukumu dhidi ya Liyumba ifikapo May 24, 2010.
Full Shangwe
0 comments:
Post a Comment