SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 28, 2010

Hujuma ya treni yaua watu kadhaa India


SARDIHA-INDIA
Kiasi ya watu 65 wameuawa nchini India kufuatia ajali ya gari moshi iendayo kwa kasi, iliyosababishwa na hujuma za waasi wa wenye kufuata itikadi za kimao.
Waziri anayehusika na usafiri wa reli nchini India, Mamata Banerjee, amesema mripuko huo mkubwa wa bomu ulisababisha gari moshi hiyo ya abiria kujibamiza katika gari moshi nyengine ya mizigo.Idadi ya watu waliokufa huenda ikaongezeka.
Vyombo vya habari nchini India vinasema kuwa takriban watu 200 walikuwa ndani ya gari moshi hiyo. Waasi hao wenye kufuata itikadi za kimao, wakiwa na maelfu ya wapiganaji waliyotapakaa zaidi katika maeneo ya mashariki na kati mwa India, kuanzia mwaka jana wamezidisha mashambulio yao.
Deutsche Welle.

0 comments:

Post a Comment