Mwanamuziki Hard Mad wa miondoko ya Reggae,Dancehall na pia Afro beat.Aliyetesa sana na
ngoma kama vile "Ni Wewe" na nyingine nyinginezo.,aachia hewani video mpya inaitwa "Mkali Ninae Mfahamu" (aka
Ujio Mpya).Na pia kuna ngoma nyingine (Audio) ambayo ameiachia inakwenda kwa jina la "Imebaki Story".
Kazi ya utengenezaji imefanywa na mtayarishaji M1 kutoka Denmark anaitwa JAKOB POLL NANDO anayesimamia kazi zake kwa sasa chini ya lebo yake inayokwenda kwa jina la MAISHA MUSIC .na video imefanywa na Adamu Juma-Visual Lab. Hivyo mashabiki wake mkae
mkao wa kula kwa ujio wake huo mpya, kila la heri man.
**************************************
RAMA D APATA SHAVU BAB KUBWA UGANDA
Msanii wa muziki wa kizazi kipya R&B Rama D toka Bongo apata shavu la kufanya corrabo na Coca Cola Pop Star wasanii Blue 3 wa nchini Uganda Kampala.Chini ya Studio za Steve Jean atagonga nao kama ngoma mbili hivi kinadada hao,Rama D ametanabaisha haya alipoongea na kituo cha Redio 88.4 Clouds FM,na tayari wanadada hao wamemtumia beat kwa njia ya internet na mtu mzima kisha andikia mashairi ya wimbo huo lakini jina la nyimbo halikuwekwa wazi kuhofia kugongana kwa mawazo na wasanii wengine. Hivyo baada ya taratibu kukamilika Rama D atachukua pipa kuelekea Kampala Uganda kwa kazi hiyo.Imetayarishwa na Ally Shaaban Mgido's.
0 comments:
Post a Comment