SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, April 28, 2010

JK ahani msiba wa watoto waliopata ajali msoga

JK akitoka katika nyumba ya familia ya Marehemu Evaristi Semeni(11) mmoja kati ya watoto watatu walifariki kwa ajali ya kugongwa na lori katika kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo,juzi jioni. JK alizitembelea familia za marehemu na kuwafariji. Semeni pamoja na wenzake Ezekiel George Setumbi(13) mwanafunzi katika shule ya msingi Mboga wilayani Bagamoyo na Omari Mrisho aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Msoga walifariki dunia baada ya kugongwa jana saa moja na nusu jioni na lori aina ya Isuzu Tiper lenye usajili wa namba SM 2514 mali ya Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo lililokuwa likitoka Chalinze Kuelekea Msata. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Bwana Mohamed Mbwana amesema kuwa wakati wa ajali hiyo mtoto Ezekiel Setumbi alifariki papo hapo ambapo wenzake Evarist Semeni(11) na Omari Mrisho(13) walifariki wakati wakipata matibabu katika kituo cha afya Chalinze. Kwa Mujibu wa Kamanda Mbwana Dereva wa lori hilo Lukino Kayela(40) mkazi wa Mji Mwema Bagamoyo amekamatwa na alitarajia kufikishwa mahakamani leo.Wanafunzi hao walifariki kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata kichwani.

0 comments:

Post a Comment