Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wa pili kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016, uliowakutanisha wadau wa Maliasili kutoka sekta binafsi na Serikalini kujadili sekta za misitu , wanyampori pamoja na mambo kale ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Eng. Angelina Madete akichangia hoja kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016.Thursday, December 1, 2016
MALIGHAFI YA MISITU HAKUNA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, December 01, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Tuesday, July 12, 2016
Women Entrepreneurship Forum
It's TIME For WOMEN With Entrepreneurship Mindset To Excel,
No Matter How The Past Was, You Can Always Begin Again.
We Are Super Excited To Welcome You For A Special Prefound Business Meeting For Women
No Matter Your Current Family, Career, Business, Challenges, You Can Soar and Achieve Your Dreams.
No Matter How The Past Was, You Can Always Begin Again.
We Are Super Excited To Welcome You For A Special Prefound Business Meeting For Women
No Matter Your Current Family, Career, Business, Challenges, You Can Soar and Achieve Your Dreams.
"A Successful Woman Is The One Who Builds A Firm Foundation With The Bricks Thrown At Her" - Unknown
Come And Soar Higher.
Come And Soar Higher.
Come & Learn A Proven Business System And Increase Your Chance Of Becomimg A Super Woman Achiever In The World.
Women Entrepreneurship Forum Special For You A Woman Aspiring For Greater Success
Women Entrepreneurship Forum Special For You A Woman Aspiring For Greater Success
When: This Saturday.
Date : 16/07/2016
Date : 16/07/2016
Time : From 3PM
Where : KING SOLOMON HALL (NEAR BEST BITES)
Entrance Fee : For Tsh. 10,000/=@
For More Info To Get Your Card Early
Call/Sms/WhatsApp Now : +255 783 149 561 Or Inbox Me?, Comment Your Number!
Minimum Number Of Seats Get Your Card Now!
Where : KING SOLOMON HALL (NEAR BEST BITES)
Entrance Fee : For Tsh. 10,000/=@
For More Info To Get Your Card Early
Call/Sms/WhatsApp Now : +255 783 149 561 Or Inbox Me?, Comment Your Number!
Minimum Number Of Seats Get Your Card Now!
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Tuesday, July 12, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
Women Entrepreneurship Forum
Monday, July 11, 2016
TANAPA YAFANIKISHA UJENZI WA ZAHANATI KATIKA KIJIJI CHA IKUZA WILAYANI MULEBA.
Diwani
wa kata ya Ikuza iliyopo katika Kisiwa cha Ikuza , wilayani Muleba mkoa
wa Kagera,Fortunatus Matta (Kulia) akimueleza jambo Meneja Mawasiliano
wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete alipoongozana
na wanahabari kutembelea kijiji hicho cha Ikuza.Wengine ni wakazi wa
kijiji hicho.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, July 11, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
KILIMANJARO COOPERATIVE BANK (KCBL) YASHEREHEKEA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA KWAKE
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, July 11, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Tuesday, June 21, 2016
MASHINDANO YA KUSOMA NA KUHIFADHI QUARAN MBAGALA BUCHA JIJINI DAR ES SALAAM
Mwanafunzi wa Madrasa AL-Mustakima Rashid Kimweli akisoma Quaran katika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quaran yaliyofanyika mbagala bucha, jijini Dar es salaam wakati wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran yaliandaliwa na Madrasa ya AL-Mustakima iliyopo Mbagala Bucha jijini Dar es salaam ambapo watoto wa kiislamu takribani 10 wenye umri kati ya miaka sita hadi 13 wa madrasa nne za Madrasa Tul – Mustakima ya Yombo Dovya, Mbagala Bucha, Madrassa Tul- ukutani na madrassa Tul Ismailia ya mtoni kijichi.
Mwanafunzi wa madrasa AL-Mustakima Zahra Mohamedi akipokea zawadi shilingi laki moja na thelathini na tano ( 135,000) kwa kuibuka mshindi wa kwanza wa kusoma na kuihifadhi juzuu tano kati ya thelathini katika kitabu cha Quaran.
Mwalimu mkuu wa Madrasa AL- Mustakima Ustaadhi Hassani Seleiman akimtunza fedha ustaadh Iddrisa wakati wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Quran yaliyoandaliwa na Madrasa AL mustakima ya Mbagala bucha jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi wa madrasa AL-Mustakima akipokea zawadi shilingi laki moja na thelathini na tano ( 135,000) kwa kuibuka mshindi wa kwanza wa kusoma na kuihifadhi juzuu tano kati ya thelathini katika kitabu cha Quaran. ( Picha na Tamimu Adam).
Na Tamimu Adam
Wazazi
na walezi wa kiislamu wametakiwa kuenzi na kuihifadhi Quran tukufu
na kuipa heshima ya aina yake kwa kuwahamasisha watoto wao kushiriki
katika mashindano ya kusoma na kuifadhi Quran ili kuwawezesha kufahamu
vizuri uislamu na kuwa muongozo katika maisha yao ya kila siku hapa
dunia na kesho ahera.
Hayo
yalisemwa na Ustaadhi Iddrisa kutoka Kigoma wakati wa mashindano ya
kusoma na kuifadhi qurani yaliandaliwa na Madrasa ya AL-Mustakima
iliyopo mbagala bucha jijini, Dar es salaam ambapo watoto wa kiislamu
takribani kumi (10) wenye umri kati ya miaka sa sita hadi kumi na tatu
wa madrasa nne ambavyo ni Madrasa Tul – Mustakima ya yombo dovya na
mbagala bucha, madrassa Tul- ukutani na madrassa Tul Ismailia ya mtoni
kijichi.
Naye
Mwalimu mkuu wa Madrasa ya AL- mustakima ambayo ndio mratibu wa
mashindano hayo Ustaadhi Hassani Suleimani alisema mashindano hayo
yalishirikisha wanafunzi kumi ambao waligawanywa katika makundi makuu
mawili kundi la kwanza ni wanafunzi watano kutoka vyuo vyote nne ambao
walisoma na kuifadhi juzuu mbili na kundi la pili ni kwa wanafunzi ambao
walisoma na kuifadhi juzuu tano.
Aidha
, aliongeza kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kuwafundisha vijana
kusoma na kuhifadhi kitabu cha mwenyezi mungu, kuipenda qurani na
kuitumia katika maisha yao yote pamoja na kuwafundisha maadili ya
kiislamu na maamurisho yake yote kwa waislamu. Aliongeza kuwa
mashindano hayo yalisimamiwa na majaji watatu kutoka mbande ambao kwa
ujumla walikuwa wanaangalia vigezo mbalimbali ikiwemo namna ya kusoma
na kutamka maneno ya quaran kwa usahihi.
Kwa
upande wake Imamu wa Msikiti wa mbagala charambe Sheikh Adam
Mikidadi ambaye alikuwa miongoni mwa majaji wa mashindano hayo alisema
kuwa mashindano yalienda vizuri ambapo yalifanyika kwa kiwango
kilichotarajiwa, washiriki walisoma na kutamka quarani vizuri kabisa na
kuweza kufikia vigezo vya mashindano kwa asilimia 85.
Sheikh
aliwataka washiriki wote kuongeza bidii mwakani ili waweze kufikia
asilimia 100 na kuwa mahiri katika kusoma, kuhifadhi na kukuza uislamu
ndani ya jamii.
Pia
aliwataka wazazi na walezi kuhamasika na kuisoma quaran tukufu ili iwe
muongozo wao katika maisha yao yote na kwa wale wenye uwezo wawe na
tabia ya kujitolewa kudhamini mashindano ya kusoma na kuhifadhi kitabu
cha mwenye mungu.
Washiriki
wa mashindano hayo walipewa zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza
Zahara Mohamed alizawadiwa shilingi laki moja na thelathini kwa kusoma
na kuhifadhi juzuu 5 kati ya juzuu thelathini na wa pili alizawadiwa
fedha taslimu elfu themanini, tano na watatu alizawadiwa shilingi elfu
sitini na tano na wengine walipewa elfu arobaini.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Tuesday, June 21, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
VOA SWAHILI: Kesi ya Mwanamama kutoka China "Malkia wa Pembe" Dar es salaam
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Tuesday, June 21, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
TANZANIA YATAJWA KATIKA NCHI ZINAZOONGOZA KWA UNYANYASAJI KWA WATU WENYE UALBINO
Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Shirika la Kimataifa la Under The Same Sun, Vicky Ntetema na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Standing Voice, Sam Clarke.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.
---
Pamoja na juhudi ambazo serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.
"Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu walio na uablino," alisema Ero.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.
"Tumejadili mambo mengi lakini tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino," alisema Nyanduga..
Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Tuesday, June 21, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Mchezo wa Shuga wabadilisha tabia za vijana
Mratibu wa mradi wa Shuga akijibu maswali yaliyokua yanaulizwa na kikundi cha wasikilizaji cha Iwawa- Makete mkoani Njombe.
Wakionyesha furaha zao baada ya kuelewa mada ya siku ukihusianisha na maisha yao ya kila siku
Mwezeshaji
wa kikundi cha wasikilizaji wa Kihesa, Manispaa ya Iringa mjini
akitimiza jukumu lake la kuelimisha wenzake na kuwawezesha kushiriki
katika majadiliano baada ya kusikiliza kipindi |
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Tuesday, June 21, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
MAPENDEKEZO YA JOPO LA JK YAANZA KUTEKELEZWA- BAN KI MOON
Na Mwandishi Maalum, New York
Umoja
wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani ( WHO), ni baadhi ya Taasisi
za Kimataifa ambazo zimeanza kutekeleza kwa vitendo sehemu ya
mapendekezo na ushauri uliotolewa na Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu
Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya.
“
Tumeanza kutekeleza baadhi ya mapendekezo ya Jopo lililokuwa chini ya
Uenyekiti wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe, Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe. Rais nakushukuru sana kwa uongozi wako, ushiriki wako na mchango
wako. Nimefarijika kwamba umeweza kuungana nasi katika mkutano huu
kutokea Senegal, kuzungumzia mapendeko ya Jopo lako”. Akasema Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Ban
Ki Moon, ameyasema hayo, jana ( jumatatu) wakati wa mkutano usio
rasmi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ulioandaliwa na Rais wa
Baraza hilo, Bw Mogens Lykketoft kwa lengo la kupokea Ripoti ya
Katibu Mkuu kuhusu uimarishaji na usanifu wa huduma za Afya Kimataifa:
utekelezaji wa mapendekezo ya Jopo la Ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa
Kimataifa wa Majanga ya Kiafya.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Tuesday, June 21, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Thursday, June 16, 2016
HABARI YA MJINI !!!
☆ Je Wajua Tuna Bonge Moja La Surprise Kwako?
☆ Je Unaipenda Gari Yako Ya Kisasa Na Nyumba Yako Nzuri? Kama Jibu Ndio, Usiwaze !!, Relax !!
☆ Ni Harufu Nzuri Ipi Ambayo Ungependa Kuivuta Wakati Unaingia Na Kuketi Ndani Ya Gari Yako Ya Kisasa Na Nyumba Yako Nzuri?
☆ Je Wajua Tuna Bonge Moja La Surprise Kwako?
☆ Je Unaipenda Gari Yako Ya Kisasa Na Nyumba Yako Nzuri? Kama Jibu Ndio, Usiwaze !!, Relax !!
☆ Ni Harufu Nzuri Ipi Ambayo Ungependa Kuivuta Wakati Unaingia Na Kuketi Ndani Ya Gari Yako Ya Kisasa Na Nyumba Yako Nzuri?
☆ Ni Wakati Wa Kufurahia Bidhaa Yetu Maridhawa Ya Forever Essential Oils.
☆ Unahitaji Forever Essential Oils !!
☆ Ifanye Nyumba Yako Au Gari Yako Kuwa Sehemu Nzuri, Kwa kutumia Mafuta Maridhawa Kutoka Forever Living, Ambayo Yatakufanya Ujihisi Hali Ya Utulivu, Bila Msongo Wa Mawazo, Ukiwa Mwenye Nguvu, Amani Na Shwari Kabisa,
Usithubutu Kuyakosa.
☆ Toa Oda Yako Sasa Utaletewa Mahali Ulipo, Free Delivery
☆ Kwa Maelezo Zaidi Jinsi Gani Nawe Unaweza Nufaika Na Bidhaa Hizi.
Call/WhatsApp : +255 783 149 561
Sms Au Inbox Me.
Email : ally.shaaban@yahoo.com
☆ Unahitaji Forever Essential Oils !!
☆ Ifanye Nyumba Yako Au Gari Yako Kuwa Sehemu Nzuri, Kwa kutumia Mafuta Maridhawa Kutoka Forever Living, Ambayo Yatakufanya Ujihisi Hali Ya Utulivu, Bila Msongo Wa Mawazo, Ukiwa Mwenye Nguvu, Amani Na Shwari Kabisa,
Usithubutu Kuyakosa.
☆ Toa Oda Yako Sasa Utaletewa Mahali Ulipo, Free Delivery
☆ Kwa Maelezo Zaidi Jinsi Gani Nawe Unaweza Nufaika Na Bidhaa Hizi.
Call/WhatsApp : +255 783 149 561
Sms Au Inbox Me.
Email : ally.shaaban@yahoo.com
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, June 16, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Monday, May 16, 2016
WCF, ILO ZATOA MAFUNZO KWA MADAKTARI 380 JUU YA NAMNA YA KUTATHIMINI AJALI NA MAGONJWA YANAYOTOKANA NA KAZI
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba akielezea malengo ya Mfuko na kazi zake, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari kwenye jengo la LAPF jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016. Mafunzo hayo yanalenga kuwaelimjsha madaktari namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, May 16, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
JENGO LA BENKI YA AZANIA MTAA WA SAMORA JIJINI DAR LANUSURIKA KUWAKA MOTO
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, May 16, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
SHUKURANI TOKA KWA FAMILIA YA ANKAL KUFUATIA MSIBA WA MWANAE MAGGID
Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi
inapenda kutoa shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa,
majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika
wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika
Kusini Jumapili ya wiki iliyopita na
kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja
mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na
kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200
kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu.
Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko
wengi mno.
Pamoja na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na
Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na
familia yao yote, Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya
Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji
Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe.
Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba
mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa. TUNAWAOMBEA
KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...
Salamu zingine za kipekee ziwaendee
watumishi wote wa Ubalozi wetu Afrika
kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa
wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban
kuja Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...
Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee
Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim
Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu
unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote. ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...
Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur
uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni
pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa watovu wa fadhila endapo
kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo
baba mfiwa Ankal ni mwanachama.
Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, Ruby 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani pamoja na Ras Makunja Na Ngoma Afrika Band wa Ujerumani na Jeff Msangi wa Canada.
TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, Ruby 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani pamoja na Ras Makunja Na Ngoma Afrika Band wa Ujerumani na Jeff Msangi wa Canada.
TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la
Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni
mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.
HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA
SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI
KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un
AMIN!
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, May 16, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
☆ Je Wajua Tuna Bidhaa Hizi Za Essential Oils? Sasa Zinapatikana!
Kampuni Ya Forever Living Product Imeleta Bidhaa Za Manukato Asilia Ya Forever Essential Oils. Yasiyo Na Kemikali Hatarishi, Yenye Ubora Na Kiwango Cha Kimataifa.
Naipenda Sana.
Tunazo Smell (Harufu) Tofauti Tofauti Kama :-
1. LEMON
2. LAVENDER
3. PEPERMINT SMELL.........
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, May 16, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
UJUMBE WA MISS TANZANIA 2016/2017 WAKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania, Lilian Kamazima mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baadhi ya wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa TBC mjini Dodoma. Kikao hicho kilijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuiomba Serikali iwasaidie kupata wadhamini wa mashindano hayo kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati wa kikao baina yao kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mjini Dodoma.
Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 mara baada kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mjini Dodoma.
Picha na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Monday, May 16, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Friday, May 6, 2016
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO YAPOKEA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.4 TOKA WHO.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari leo 6 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam kuhusu msaada walioupokea toka Shirika la Afya Duniani (WHO) wenye thamani ya shilingi bilioni 1.4.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro wakikabidhiana hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro (kulia) akikabidhi jokofu kwa kwa jaili ya huduma za chanjo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa juu ya makabdhiano ya vifaa tiba toka Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo 6 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Benedict Liwenga)
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutoa chanjo kwa akina mama na watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali nchini.
Akiongea na waandishi wa habari Wizarani hapo, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dkt. Neema Rusibimayila ameeleza kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia uhifadhi wa chanjo katika mikoa mbalimbali pamoja halmashauri nchini.
‘’Ni msaada mkubwa tulioupata toka WHO na nina amini kuwa utatusaidia sana katika kufanikisha suala la chanjo kwa akina mama na watoto nchini na pia tunaamini wataendela kushirikiana na Wizara ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea’’, alisema Dkt. Rusibimayila.
Ameongeza kuwa, kwa sasa vituo vipya vinavyofunguliwa nchini vikiwemo vile ambavyo havikuwa na majokofu vitakuwa na uwezo wa kupata vifaa hivyo kama vile majokofu na vifaa vingine vya tiba ili huduma za chanjo ziweze kutolewa katika kila kituo nchini.
Akikabidhi vifaa hivyo Wizarani hapo, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ni pamoja na majokofu 200 pamoja na vifaa vitumikavyo kwa ajili ya kutolea chanjo.
Kwa upande wake Mratibu Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana Emmanuel Yohana ameeleza kuwa, majokofu hayo pia yatapelekewa katika wilaya ambayo yana upungufu wa majokofu pamoja na vituo vipya kwa ajili ya kupunguza umbali kwa wagonjwa wa chanjo na pia ni moja ya kuweka huduma karibu na wananchi nchini.
Aidha, ameongeza kuwa spesimeni za polio na surua zilizotolewa na WHO zitapalekwa pia katika vituo kwa jili ya kuchukua damu kwa ajili ya vipimo na kuletwa Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi wa maabara.‘’Wanufaika wa huu msaada kutoka WHO ni wananchi wote wa Tanzania kwani utaenda katika vituo vyote vya chini zikiwemo Zahanati’’, alisema Yohana.
Kupitia wadau mbalimbali Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kushirikiana na wadau hao katika kutafuta vifaa tiba mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa sekta ya afya nchini inaimarika kwani Tanzania kwa sasa imeweza kudhibiti polio kwa kiasi kikubwa.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Friday, May 06, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Thursday, May 5, 2016
WELCOME TO A BIG EVENT SATURDAY - EAGLE MANAGER LAUNCH "ROCK THE BOAT"
Tutakuwa Na Special Launch Ya Eagle Manager Incentive Jumamosi Hii.
Tarehe 7/05/2016 Mahali UBUNGO PLAZA Kuanzia Saa 8 Kamili SHARP Mchana.....
Kwa Kiingilio cha 5000/=@ Tu.......!
Napenda Kukukaribisha Kwenye Mafunzo
Yatakayo Kuwezesha Ujifunze Na Kukupa Njia Ni Namna Gani Na Wewe Unaweza Ukafikia Vigezo Vya Kuipata Safari Ya Kusafiri BURE Bila Kulipa Chochote FULL PAID (Umelipiwa Kila Kitu) Mwakani Mwezi Wa 9....... ROME-ITALY, MONTE CARLO Na BARCELONA!!
Je Ungependa Kujiunga Nasi Kwenye LIKIZO Ndani Ya meli Kubwa Ya Kifari CRUISE SHIP Ya "FREEDOM OF THE SEAS" Mwakani? 0 Hii Itakupa Tiketi Mbili Unaweza Kwenda Na Umpendae, Utalipiwa 5 Star Hotel, Chakula Michezo Na Pocket Money!!
Safari Itakupatia Fursa Ya Kutembelea Miji 3 Mashuhuri Duniani...Tutaanzia Barecelona, SPAIN -Tutaelekea- Monte Carlo, MONACO - Halafu Tutamalizia Na Rome, ITALIA Na Kurejea Tena Bercelona........ Vipi? Unahisi Inakuhusu Hii? 5 Star Treatment?
Unayo Nafasi Na Mwezi Huu Ndio Mambo Yanaanza
Usithubutu Kukosa Hii.........
Text/ Namba Yako Kwenye Namba
+255 783 149 561 Ama Whatsapp
Kuweza Hudhuria.........
KARIBU!
+255 783 149 561 Ama Whatsapp
Kuweza Hudhuria.........
KARIBU!
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, May 05, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
NSSF YAZIDI KUZOA WANACHAMA WAPYA
Wananchi wa maeneo ya Banana jijini Dar es Salaam wakiwa katika foleni ya kujiandikisha na kujiunga na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF ambapo jumla ya wanachama 160 walijiandikisha katika eneo hilo. Katika eneo la Mwembeyangawanachama wapya 214 walijiandikisha na Mbagala 132 na kufanya jumla ya wanachama wapya 506 walijiandikisha.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, May 05, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Wateja Wa KLM Sasa Kununua Tiketi Kwa M-Pesa
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na
makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(Kushoto
aliyekaa)na Meneja mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad
Khuller(kulia)wakisaini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya wateja wa
KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-Pesa,Mkataba
huo ulisainiwa jijini Dar es Salaam leo,Anaeshuhudia katikati ni
Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom
Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit.
Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom
Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit(katikati)akishuhudia
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na
makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(Kushoto)na
Meneja mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad Khuller
wakibadilishana mikataba baada ya kuisaini kwa ajili ya wateja wa
KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-Pesa,Hafla
hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na
makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(Kushoto)na
Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad
Khuller(kulia)wakielekeza jinsi ya kukata tiketi kupitia huduma ya M-
PESA na Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom
Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit(katikati) wakati wa hafla
ya kusainiana mkataba kwa ajili ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao
za kusafiri kupitia huduma hiyo,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam leo.
Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad
Khuller(kulia)akimsisitiza jambo Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha
huduma za kibiashara na makampuni wa Vodacom
Tanzania,Gregory Verbond,baada ya kusainiana mkataba kwa ajili
ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-
Pesa,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye
picha ya pamoja na Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa
Vodacom Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit(kushoto) Ofisa
Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na
makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(wanne toka
kushoto)pamoja na Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM
nchini,Sharad Khuller(watano toka kushoto) wakati wa hafla ya
kusainiana mkataba kwa ajili ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao za
kusafiri kupitia huduma ya M-PESA,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam leo.
Wateja
wa Shirika la ndege la Uholanzi la KLM watakaokuwa wanatumia usafiri wa
anga kuanzia sasa wataweza kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia
huduma ya M-Pesa,Hiyo imekuja baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya
kutoa huduma hiyo kwa Kampuni hiyo na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania leo.Huduma hii imekuwa inatumiwa na makampuni mbalimbali
kupokea malipo na kuwarahisishia wananchi maisha.
Wateja
wa shirika la KLM pia sasa wataweza kulipia huduma mbalimbali kupitia
M-Pesa badala ya kupoteza muda kutembelea ofisi za shirika hilo na
mawakala wake baadhi ya huduma hizo zikiwa ni kununua tiketi za
safari,kulipia mizigo ya ziada,malipo ya kuahirisha safari.
Akiongea
kuhusu ushirikiano huu Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za
kibiashara na makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond,alisema
“Tunayo furaha kufanya kazi na shirika la KLM ambapo sasa wateja wetu
maisha yao yamezidi kurahisishwa sasa wanaweza kupata huduma za shirika
hili kupitia simu zao za mkononi kwa kufanya malipo kwa M-Pesa”.
Verbond
aliongeza kuwa mtandao wa M-Pesa hivi sasa unatumiwa na taasisi na
makampuni mbalimbali ya serikali na binafsi katika kurahisisha kupokea
malipo kwa urahisi kutoka kwa wateja wao na imethibitika kuwa njia
inayorahisisha maisha,kuokoa muda na ni salama.
Aliyataja
baadhi ya mashirika ya ndege ambayo kwa sasa wateja wake wanafanya
malipo kupitia huduma hii kuwa ni Qatar Airways, Precision Air, Kenya
Airways, Air Tanzania, Fast Jet, Eagle Air na Auric Air.
Kwa
upande wake Meneja wa Shirika la KLM nchini,Sharad Khuller alisema kuwa
wamejiunga na huduma ya M-Pesa kutokana na maombi ya wateja wake
katika kuwarahishia maisha kwa kulipia huduma wanazohitaji hususani
kununua tiketi za safari za kwenda nchi mbalimbali duniani,Huduma kwa
wateja kwa kampuni yetu ni kitu muhimu sana kwa KLM.
Ushirikiano
huu na Vodacom Tanzania kupitia huduma ya M-PESA ni njia muhimu sana
kwa kutoa huduma zilizo bora kwa wateja wetu ni huduma inayowafanya
wateja wawe huru kwa kulipia tiketi zao kwa haraka na bila
usumbufu,alisema Khuller
Kupata
huduma hii anachopaswa kufanya mteja ni kupiga namba*150* 00#,ambapo
kwenye menu ya simu yake atachagua huduma namba 4 inayoelekeza kulipa
kwa M-Pesa,baadaye atachagua huduma namba 3,kuchagua aina ya biashara ni
namba 9,kisha atachagua namba 3 inayoonyesha huduma za usafiri na
mwisho atachagua KLM
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, May 05, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
RITA yaanza kukusanya ada za usajili kwa njia ya kielekroniki
Serikali
inaendelea kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ili kuchangia upatikanaji
wa fedha za kusaidia kuimarisha na kuendeleza miradi ya maendeleo
nchini.
Wakala
wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imekuwa miongoni mwa taasisi za
Serikali ambayo imeanza kukusanya ada zote zitokanazo na huduma inazotoa
kwa njia ya kielekroniki kwa wadau wake kufanya malipo kwa njia ya simu
au benki kabla ya kupata huduma wanayohitaji.
Hayo
yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria,
Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akiwasilisha mpango wa makadirio ya
bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
“Tayari
wilaya 114 kati ya 139 zinakusanya maduhuli kwa njia ya kielekroniki na
kwamba ifikapo Juni, 2016 wilaya zote Tanzania Bara zitakuwa zinatumia
njia ya kielekroniki kukusanya maduhuli,” alisema Dkt. Mwakyembe.
Katika
kuongeza mapato, Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa upo mkakati wa kuongeza
kiwango cha usajili wa vizazi na vifo nchini, ambapo RITA imeanzisha
kampeni ya usajili inayoambatana na uboreshaji wa mfumo wa usajili kwa
kuweka mfumo wa kompyuta kila wilaya ambapo kampeni hizo zilifanyika.
Wilaya
ambazo kampeni hizo zimefanyika ni Arusha na Arumeru ambapo jumla ya
watu 49,548 wamesajiliwa na kupewa vyeti vyao vya kuzaliwa.
Zoezi
hilo la usajili linaendelea katika wilaya ya Kahama na baadaye
litaendelea katika wilaya 16 nchini ambazo ni Bariadi, Chato, Dodoma,
Igunga, Kilombero, Kilosa, Lushoto, Maswa, Mbinga, Misungwi, Mtwara,
Muleba, Nzega, Shinyanga, Sumbawanga na Tunduru.
Waziri
Mwakyembe alibainisha kuwa Wizara hiyo kupitia RITA imekusudia kusajili
zaidi ya watu 500,000 katika maeneo hayo na kupatiwa vyeti vya
kuzaliwa.
Kwa
mujibu wa utafiti wa afya uliofanyika 2010, asilimia 16 ya watoto wenye
umri wa miaka mitano ndio wenye usajili na vyeti vya kuzaliwa Tanzania
Bara ikilinganishwa na Tanzania Zanzibar ambapo usajili ulikuwa ni
asilimia 79.
Ili
kukabiliana na hali hiyo, RITA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wamebaini mradi wa kusajili watoto
chini ya umri wa miaka mitano uliofanyiwa majaribio wilaya ya Temeke
mwaka 2012 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2014 mkoani Mbeya.
Kampeni
hiyo imeonesha mafanikio na tija kwa taifa ambapo usajili umeongezeka
na kufikia asilimia 58 ambapo awali mkoa wa Mbeya usajili ulikuwa
asilimia 8.7.
Kampeni
hiyo ni endelevu kwa nchi nzima ambapo mikoa itakayoanza kufanya
usajili ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Iringa, Njombe,
Tabora, Kagera na Dodoma.
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, May 05, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
TANAPA KUBADILI MFUMO WA UTENDAJI KAZI KUTOKA KIRAIA KUWA JESHI USU
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Allan Kijazi (kulia) akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuelekea katika uwanja wa Mafunzo katika kambi ya Mlele kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Wahifadhi na Askari wapya waajiriwa wa shirika hilo .
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipiga saluti wakati akipokea salamu za heshima wakati wa gwaride maalumu la ufungaji wa mafunzo ya awamu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride la heshima la askari wapya na Wahifadhi waliohitimu mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa mwendo wa pole na kutoa heshima wakati ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa jeshi usu kwa Wahifadhi
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipiga saluti wakati gwarde likipita mbele ya jukwaa na kutoa heshima,wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori, Martin Loibooki,Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa, Allan Kijazi, Kaimu Mkurugenzi idara ya Wanyama pori, Ndugu Karamaga.
Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa mwendo wa haraka wakati ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi
Askari wapya waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakionesha umahiri katika kutumia silaha wakati wa kukabiliana na majangili mara baada ya kupata mafunzo hayo katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.
Baaadhi ya Wahifadhi Waandamizi na Wafawidhi wakiwa wameshika silaha mara baada ya kupatiwa Mafunzo katika Kambi ya Mlele ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kwenda Jeshi Usu.
Askari wa Hifadhi akionesha umahiri katika matumizi ya silaha kwa kulenga shabaha wakati wa kuhitimu mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi
Baadhi ya Viongozi na Wageni katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na askari waajiriwa wakifuatilia maonesho yaliyokuwa yakifanywa na wahitimu hao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete (kulia) akiratibu shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Asakari Waajiriwa .kushoto ni Mkuu wa Mafunzo ,Genes Shayo .
Mhifadhi Sekela
Mwangota akisoma risala ya Wahitimu wa
Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa mgeni rasmi ,Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili
na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha
mafunzo hayo kwa wahifadhi na askari wapya waaajiriwa wa shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) yaliyofanyika kwenye kambi ya Mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Mwangota akisoma risala ya Wahitimu wa
Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa mgeni rasmi ,Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili
na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha
mafunzo hayo kwa wahifadhi na askari wapya waaajiriwa wa shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) yaliyofanyika kwenye kambi ya Mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori,Martin Loibooki akizungumza wakati wa hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Asakari Waajiriwa .
Baadhi ya Wahitimu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati waa hafla ya ya ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari Waajiriwa .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu ,Raphael Muhuga akizungumza hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari Waajiriwa ambapo amegusia juu ya changamoto iliyopo kwa Wafugaji kuingiza Mifugo yao katika Hifadhi pamoja na mapori ya Akiba.
Katibu Mkuu ,Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitoa hotuba yake ya kuhitimisha Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA),Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Baadhi ya Askari Waliohitimu.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi za Taifa(TANAPA) yaliyofanyika kambi ya mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyeko Katavi.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Thursday, May 05, 2016
0
comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook