SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.
Showing posts with label TAARIFA MAALUM KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:TAARIFA UHUSU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE “DENGUE FEVER”. Show all posts
Showing posts with label TAARIFA MAALUM KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:TAARIFA UHUSU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE “DENGUE FEVER”. Show all posts

Friday, February 7, 2014

TAARIFA MAALUM KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:TAARIFA UHUSU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE “DENGUE FEVER”


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
  Utangulizi

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma juu ya kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya dengue yaani “dengue fever” hapa nchini. Ugonjwa huu umethibitishwa baada ya sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa watu waliohisiwa kuwa na ugonjwa huu jijini Dar es salaam kupelekwa kwenye maabara yetu ya Taifa Dar es salaam na kuthibitisha kuwa na virusi vya homa ya dengue mnamo mwishoni mwa mwezi wa Januari. Hadi sasa idadi ya wagonjwa ambao wamethibitishwa kuwa na ugonjwa huu ni
 21 na hakuna mgonjwa yeyote aliyepoteza maisha. 

Homa ya Dengue