SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, January 1, 2015

Salaam Za Mwaka Mpya Kutoka Kwa Maggid Mjengwa

1_20c9c.jpg

Kwangu mwaka 2015 nadhamiria uwe ni wa kusonga mbele zaidi. Na ningependa sote tuwe na dhamira hiyo ya kusonga mbele kama watu binafsi na kama taifa. Tutangulize zaidi maslahi mapana ya nchi yetu.
Kama ilivyokuwa mwaka uliomalizika, mwaka 2015 nitapenda nijikite zaidi kwenye kuhamasisha juhudi za maendeleo kwa Wanawake na Vijana wa Vijijini. Nitapenda pia niimarishe Jukwaa la ' Kwanza Jamii Dialogue' kwa maana ya mijadala ya wazi kuhusiana na masuala muhimu ya kitaifa.
Ni kwa kupitia KwanzaJamii Radio pia. Ni kwa kuwahakikishia
watembeleaji wa Mjengwablog na wasikilizaji wa KwanzaJamii radio mtandaoni kuwa tutakuwa wa kwanza kuwaletea habari za kichambuzi kuanzia saa kumi na moja na nusu alfajiri. Ni kwa kuwaletea magazeti ya siku husika, na kuyachambua pia. Kwenye Mjengwablog na KwanzaJamii Radio.
Hivyo basi, kuimarisha concept yetu ya ' Soko la Habari Kariakoo'.
Mapya mengine?
Tutawaletea kipindi kipya cha ' Mwangaza wa Watanzania Diaspora'. Kipindi kingine ni cha ' Football Baraza'. Yepi yatakuwamo ndani? Usikose kutufuatilia kuanzia kesho Januari Mosi, 2015.
Naam, nitapenda kujikita kwenye yale yenye pia kuibua mijadala endelevu kwa maendeleo ya nchi yetu.
Pamoja na yote hayo, mwaka 2015 nitajitahidi, kama mzazi, kutenga muda zaidi wa kuwa na familia yangu; mke wangu mpenzi na wana wangu.
Nawatakia nyote HERI YA MWAKA MPYA!
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252

0 comments:

Post a Comment