SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, May 23, 2014

MTOTO WA MIAKA MINNE (4) ASHEREHEKEA BESDEI YAKE YA KUZALIWA MLIMA KILIMANJARO

Mtoto Aldof Isack (4)akikata keki wakati wa sherehe ya kumbukumbu yasiku yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika kilele cha Shira Mlima Kilimanjaro ,Kilele chenye urefu wa mita 3,850 ambazo ni sawa na futi 12,630.aliyepiga magoti ni mama wa mtoto huyo Jackline Mchila na nyuma ya mtoto ni dada yake,Feith Isack huku baba yao kushoto akiwa ameshikachupa ya Champagne

Baba wa mtoto Adolf Isack,Bw Isack Kalage akifungua Champagne wakati wa shrehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtoto wake huyo aliyetimiza miaka minne(4),sherehe iliyofanyika katika kilele cha Shira mlima Kilimanjaro.
Mtoto Adolf Isack akikata keki huku akiimbiwa na watalii wa ndani mbalimbali waliopanda mlima Kilimanjaro wakiwemo wazazi wake.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini. 

WAZAZI wa mtoto Aldof Isack (4) wametumia fursa iliyotolewa na hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro ya kupanda katika kilele cha Shira kwa gharama nafuu kuandaa sherehe ya kuzaliwa ya mtoto huyo katka kilele cha Shira. 


Wakiwa miongoni mwa kundi la pili lililopanda mlima huo kupitia njia ya Londros wazazi hao ,Isack Kalage na Jackline Mchila wakiwa na watoto wao wawili Adolf Isack na Feith Isack pamoja na ndugu wengine walifanya sherehe hiyo ambayo iliwaacha watu na mshangao. 


Akizungumzia tukio hilo la aina yake kutokea katika mlima huo baba wa mtoto huyo ,Kalage alisema aliamua kufanya sherehe hiyo ikiwa sehemu ya kuutangaza utalii wa ndani wa mlima Kilimanjaro pamoja na kuweka kumbukumbu kwa mtoto huyo ya kukumbuka siku yake ya kuzaliwa akiwa na miaka minne akiwa Mlima Kilimanjaro. 


“Kila mwaka watoto wangu wanapo fanya vizuri katika masomo yao huwauliza ni wanataka niwafanyie …na safari hii baada ua Aldof kufanya vizuri huko shuleni kwake Mother Theresa aliomba kupelekwa mbugani lakini baada ya kusikia ofa iliyotolewa na KINAPA ,ilibidi tubadilishe ili tufanyie Birthday yake huku mlimani kama sehemu ya kumbukumbu”alisema Kalage. 


Alisema amekuwa kila mwaka akiwapeleka watoto wake hao katika hifadhi mbalimbali za taifa zikiwemo sehemu za kihistoria kama Zanzibar ili kuwajengea watoto wake hao mazoea ya kutembelea vivutio vilivyopo nchini pindi wawapo watu wazima. 


Kwa upande wake mhifadhi Helen Mchacky aliyekuwa ameambatana na kundi hilo alisema  utaratibu huu wa kupandisha watalii wa ndani katika maeneo hayo ya vivutio katika mlima Kilimanjaro utakuwa endelevu huku akitoa wito kwa familia ,taasisi mbalaimbali kutumia fursa hiyo kujifunza historia . 


“Nje ya Ofa hii tuliyotoa bado ipo nafasi kwa taasisi ,vikundi ama
familia kupanda Mlima Kilimanjaro kwa gharamu ambazo ni nafuu sana hasa kwa wakazi wa Afrika Mashariki kikubwa na kutenga muda na kujiandaa na kuja kutizama vivuto hivi”alisema Mgungusi.
Mwisho.


NA ANKAL MICHUZI