SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, March 8, 2014

Makamu wa Rais Dkt. Bilal aomboleza kifo cha mtoto wa Waziri Sophia Simba, Dar

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, kutoa pole. (Picha na OMR).
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwake  Masaki jijini Dar es Salaam, kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika leo kwenye Makaburi ya Kinondoni. 
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, jana kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika leo kwenye Makaburi ya Kinondoni. 
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa, Waziri mstaafu (wa pili kulia) Mjumbe wa Nec Wilaya ya Busega, Chegeni (kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, wakizungumza jambo wakati wakijumuika kwa pamoja katika maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, Masaki jijini Dar es Salaam.
5
6
Baadhi ya waombolezaji.(Picha na OMR).

0 comments:

Post a Comment