SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, March 10, 2014

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Apokea magari mawili kwa ajili ya mafunzo ya udereva

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasha gari ya kuinulia mizigo focal lift kama ishara ya kupokea moja ya magari mawili yaliyokabidhiwa na Shirika la Transaid la nchini Uingereza kwa Chuo cha Taifa cha Usafirshaji (NIT), leo asubuhi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt.  Zakaria Mganilwa
Taswira ya tanker trailer la futi 40 na Folk Lift ambayo yamekabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) na Kampuni ya Transaid leo asubuhi katika viwanja vya chuo hicho. Magari hayo yatasaidia wanafunzi wanaosoma kozi za udereva chuoni hapo.
      Mkurugenzi wa Mradi ya Usalama Barabarani wa Shirika la Transaid la Nchini Uingereza, Mr. Neil Rettie (mwenye tai ya blue) akimkabidhi funguo za gari aina ya Iveco kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka kwa ajili ya mafunzo ya Udereva yanayotolewa na Chuo Cha Taifa Cha Usafirhsaji (NIT), Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya chuo hicho leo Asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka, akiwasha gari aina ya Folk Lift lililokabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usarifshaji (NIT), kwa ajili ya wanafunzi wataochukua mafunzo ya udereva chuoni hapo. Magari hayo yamekabidhiwa leo asubuhi katika viwanja vya Chuo hicho.
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa ajili ya kufundishia mafunzo ya udereva chuoni hapo, magari hayo yalimekabidhiwa leo asubuhi na Shirika la Transaid la nchini Uingereza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa ofisini kwake kabla ya kupokea magari mawili ambayo yamekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Transaid la nchini Uingereza, hafla ya kukabidhi magari hayo imefanyika leo asubuhi katika viwanja vya NIT.Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi

0 comments:

Post a Comment