Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne Mcintosh, akizungumza na
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz
Afrika katika mpango mkakati wa kubadilishana nao mawazo na uzoefu
katika shughuli za biashara na masoko katika ukanda wa Afrika.
Wakuu
wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz
ukanda wa Afrika ni kutembelea kampuni hiyo kubwa na ya siku nyingi ya
magari hapa duniani na kuangalia aina mpya za bidhaa ambazo zipo sokoni
na kupata kujifunza kazi mbalimbali za kijamii ambazo kampuni hiyo ya
CFAO Motors inafanya hapa Tanzania.
Wakuu
wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz
Afrika kutoka nchi za Rwanda, Sudan, Afrika Kusini na nchi zingine
wamekuja nchi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na wamefanikiwa kujifunza
shughuli mbalimbali za ufundi na utendaji kazi wa kampuni ya CFAO
Tanzania.
Wakuu
wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz
Afrika pia walipata fursa ya kuangali akarakana ya kampuni hiyo kwenye
maeneo ya Vingunguti na kuona shughuli za ufundi kwa magari yao ambapo
wateja ambao wanaharibikiwa na magari wanaweza kupata huduma hiyo kwenye
karakana ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
wa Biashara wa CFAO Motors, Charles-Edouard CAMBOURNAC akitoa maelezo
kwa Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes
Benz Afrika.

Wakuu
wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz
Afrika wakitembelea eneo linalotoa huduma ya kutengeneza kwa teknolojia
ya hali ya juu magari ya wateja wa kampuni hiyo pindi yanapopata
hitilafu.

Baadhi ya magari ya wateja wa Kampuni ya CFAO Motors yakisubiri kuhudumiwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CFAO Motors, Wayne Mcintosh (katikati) akibadilishana
mawazo na Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors, Charles-Edouard
CAMBOURNAC, wakati wa Ziara ya kujifunza kutoka Wakuu wa Mercedes Benz
kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika. Kushoto ni
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed.
Wakuu
wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz
Afrika wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufika makao makuu ya
kampuni hiyo.
Baadhi
ya kikundi cha wamasai walioburudisha Wakuu wa Mercedes Benz kutoka
Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika kwa kucheza ngoma za
Kimasai.

Baadhi
ya Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes
Benz Afrika wakichukua kumbukumbu za matukio kwenye simu zao wakati
kikundi cha Kimasai kilipokuwa kinatoa burudani.

Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed akifurahi jambo na mmoja wajumbe hao.




0 comments:
Post a Comment