Francis Cheka
Unajua kwamba Star wako Francis Cheka ni mtoro shuleni?? Licha ya kuamua kurudi shule, mwalimu anayesimamia programu ya bondia Francis ‘SMG’ Cheka, James Mkisi amesema bondia huyo aliingia darasani siku moja tu tangu aliposajiliwa kama mwanafunzi mpya wa Chuo cha St Joseph cha mjini Morogoro Septemba mwaka jana.
Mwalimu Mkisi alisema juzi kuwa bondia huyo ameomba kuendelea na masomo baada ya kutoonekana darasani kwa miezi kadhaa bila taarifa yoyote na kubainisha kuwa hawawezi kumruhusu kuingia muhula wa pili na kueleza endapo bondia huyo anahitaji kuendelea na masomo atalazimika kujisajili kama mwanafunzi mpya.
Cheka alipewa ufadhili wa masomo chuoni hapo mwaka jana mara baada ya kutwaa ubingwa wa dunia wa WBF Agosti 30 baada ya kumpiga Phil Williams wa Marekani katika pambano lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkisi alisema bondia huyo amekosa vipindi kwa muda mrefu hivyo hawezi kuingia muhula mwingine kwani atakosa vitu vingi hivyo anapaswa kujisajili kama mwanafunzi wa muhula mpya utakaoanza Machi 24.
“Cheka aliingia darasani siku moja na ‘kupotea’ hata hivyo hivi karibuni alikuja na kutuambia anataka kuendelea na shule ingawa hatuwezi kumuendelezea programu yake ya awali,” alisema Mkisi.
BOFAYA HAPA




0 comments:
Post a Comment