Ujasiriamali
ni jambo lililojema miongoni mwa jamii. Watu wengi wamekuwa
wakilalamika kukosa vitu vya kufanya ili kuweza kujipatia kipato na
kuacha kuwa tegemezi kwa wazazi au waume na hata wakati mwingine wake
zao. Wana dada wawili marafiki ambao kwa bahati majina ya ubini ya
wazazi wao yanafanana na wao kuamua kujiita ndugu, Joan Joseph Massawe
(pichani kulia) na Angel Fabian Massawe wao kwa kuliona hilo waliamua
kuanzisha bishara ambayo itawapatia kipato cha ziada mbali na ajira zao
nma kuwasaidia katika masomo yao.
Wakiuambia
mtandao huu wa Father Kidevu Blog kuwa wao ni wasomi na wameamua
kuopika vitafunwa vya aina mbalimbali na kuviuza na pia wamekuwa
wakifanya hivyo katika tafrija mbalimbali kwa kupika bite.
Muiongoni
mwa vitu ambavyo leo viilivuta FK Blog hadi katika meza ya wana dada
hao 'The Ladies' iliyopo katika maonesho ya Tamasha la Mwanamke na Akiba
ndani ya Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam ni vitumbua. Yes
Vitumbua hivi hivi, maana ni vikubwa na vinamvuto. Lakini pia katika
meza yao kulikuwa na vitu vingi kama chapati za maji na kusukuma,
sambusa, kababu, kalimati, na kalimati.
Wanadada
hawa ni mfano wa kuigwa kwa namna ambavyo waliamua kubuni biashara
hiyo. Na niwazi kuwa hata hapo baade wakiwa na kampuni kubwa ya biashara
hii sitaweza jkushangaa.
Pichani
ni Angel na Joan wakiwahudumia wake wa viongozi mbalimbali wakiongozwa
na Mke wa Makamu wa Rais mama Asha Bilali aliyekuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi wa tamasha la Mwanamke na Akiba.
Angela na Joan wakimhudumia mama Asha Bilali vitumbua hivi ambavyo leo navizungumzia.
Hakika kila mama aliyepita katika banda hilo hakuacha kununua kitafunwa.
Vitumbua hivyoooo kazi kwenu wana dada hawa wanapatikana Oysterbay barabara ya Bongoyo.
MAWASILIANO ZAIDI KWA WENYE UHITAJI:
+255 713 185065 AU +255 652 035652
0 comments:
Post a Comment