Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa(UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akisoma Ujumbe kutoka
kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon na Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Bi Irina Bokova katika Maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani.
Mshehereshaji Meneja
wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania( MCT), Bw. Allan Lawa,
akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya siku ya Redio
Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma. Maadhimisho hayo
yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na kufadhiliwa na
UNESCO.
Na Mwandishi Wetu, Moblog Tanzania, Dodoma
UMOJA wa Mataifa umesema kwamba bado
redio nyingi duniani ziko nyuma katika kuhabarisha habari za usawa wa
jinsia na sauti za wanawake na wasichana hazipati nafasi ya kutosha
katika matangazo ya kila siku katika vyombo vingi vya habari.
Akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Bw, Ban Ki-Moon na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Irina Bokova, katika
maadhimisho ya siku ya Radio Duniani jijini Dodoma, Afisa Habari wa
umoja wa Mataifa, Bi Usia Nkhoma Ledama amesema mbaya zaidi katika bodi
za mashirika ya vyombo vya habari wanawake ni robo tu ya wanabodi.
“Ninavihimiza vituo vya redio kuwatambua kwa usawa wanawake kama wafanyakazi na kama wasikilizaji wake,”
“Maadhimisho ya mwaka huu
yanatukumbusha wajibu wa watangazaji wa redio duniani kote kuipaza sauti
ya wanawake na kuthamini nafasi ya wanawake katika mashirika ya
utangazaji,” akisoma taarifa hiyo
Bi Usia akisoma taarifa hiyo amesema
Radio pia inaweza kusaidia sana kumaliza unyanyapaa dhidi ya wanawake na
programu zisizozingatia usawa wa kijinsia kwa wote.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema
Nchimbi akisalimiana na Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco, Mama
Rose Haji Mwalimu meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya Redio
Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma. Katikati ni Katibu Mtendaji
wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga.
Amesema kwenye hotuba hiyo ya wakuu wa
Umoja wa Mataifa kwamba hii ni fursa kwao wote, kusherehekea Siku Ya
Radio Duniani kwa kuwatambua wanawake na kufanya yale yaliyo ndani ya
uwezo wao kuzilea sauti mpya za kesho.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa
UNESCO Bi Irina Bokova amesema na ninanukuu; Katika Siku ya Redio
Duniani, tunaadhimisha chombo ambacho kinategemewa zaidi na watu wengi,
wanaume kwa wanawake, duniani kote. Redio huwapa sauti wale wasio na
sauti, husaidia kuelimisha watu wasio na elimu, na inaokoa maisha wakati
wa majanga.
Akisoma taarifa hiyo amesema ikiwa ni
chachu ya uhuru wa kujieleza na ushirikishwaji wa wengi, redio ni muhimu
katika kujenga jamii yenye uelewa na kukuza heshima na uelewano baina
ya watu.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari
(MCT), Bw.Kajubi Mukajanga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi.
Ujumbe huo wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO
ulisisitiza kwamba Radio ni muhimu zaidi katika kukuza usawa wa
kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
“Tangu wakati wa watendaji waanzilishi
mwanzoni mwa karne ya 20 hadi hawa wa sasa wanaoripoti kutoka kwenye
maeneo yenye vita, wanawake wamefanya kazi kubwa katika ukuaji wa
redio,Kama waandishi wa habari wa kiraia, maripota, watengenezaji
vipindi, mafundi, na watu muhimu wanaofanya maamuzi, wanawake wanafanya
kazi katika kila ngazi ya sekta ya utangazaji kuhakikisha ubadilishanaji
huru wa maoni, habari na mawazo kupitia masafa,” ilisema taarifa hiyo.
Bi Usia amesema kupitia ujumbe huo
kwamba ni kwa sababu hiyo UNESCO inafanya kazi duniani kote kuendeleza
radio kama chombo huru na kinachoshirikisha watu wengi kwa ajili ya
wanaume na wanawake, na kutengeneza mazingira salama zaidi kwa waandishi
wa habari wote, kwa kutambua kwa namna ya pekee vitisho kwa waandishi
wa habari wanawake.
Pichani juu na chini ni Mgeni rasmi
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza na wadau wa
sekta ya Habari nchini kwenye maadhimisho ya siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr.Rehema Nchimbi ambaye aliwaasa
waandishi kutangaza vipindi vyenye manufaa kwa jamii ili kusaidia
kusukuma maendeleo.
“Tungependa kusikia vipindi vya maendeleo zaidi katika redio kuliko vipindi vya muziki,”alisema
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la
Habari (MCT)Kajubi Mukajanga alisema maadhimisho hayo yamewashirikisha
washiriki kutoka nchi nzima na yanalenga kuwakumbusha wajibu
watangazaji wa redio juu ya nafasi ya radio katika kuelimisha jamii.
Mchokonozi wa Mada na Mkufunzi wa
Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu akiwasilisha mada
inayosema kutumia fursa ya Redio kukuza usawa wa Kijinsia na kuwawezesha
Wanawake katika Uongozi.
Meneja Machapisho, Utafiti na Uhifadhi
Hati wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mireny, akitoa
maelezo mafupi kuhusu machapisho mbalimbali ya baraza hilo yanayotoa
mafunzo mbalimbali ya tasnia ya habari.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akizindua machapisho ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwenye maadhimisho ya siku ya Redio Duniani. Kushoto ni Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu na Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT), Bw.Kajubi Mukajanga.
Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Habari,
Watangazaji na waandishi wa Redio za Jamii nchini wakiwa kwenye
maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani
Dodoma.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifuatilia yaliyokuwa
yakijiri kwenye maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani.
Wadau wa UNESCO na MCT.
Baadhi ya waandishi wa habari wa Redio
za jamii nchini na wadau wa sekta ya habari wakichangia maoni wakati wa
majadiliano ya kuzungumzia changamoto zinazozikabili redio za jamii
nchini.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Dkt. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya
habari walihudhuria maadhimisho ya siku ya Redio duniani yaliyofanyika
Kitaifa mkoani Dodoma kwa mara ya kwanza.





















0 comments:
Post a Comment