Dr
Ellen Otaru Okoedion Private Sector Development Programme 2013 Team
leader from Tanzania, takes participants through a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- launch in Dar es Salaam to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses.
Dr
Ellen Otaru Okoedion Private Sector Development Programme 2013 Team
leader from Tanzania, introducing her teammates who also participated in
the launch of a new website-www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. The ceremony was held in Dar es Salaam at the weekend.
Malena
Rosman, Head of Development Cooperation Division in the embassy of
Sweden (holding a flower boutique and wearing a red jacket) in a group
photo with Private Sector Development (PSD) Programme 2013 Team shortly
after their graduation and launch of a website to help
local entrepreneurs formalize and grow their businesses. Far left is
Julia Norinder and far right is Daniel Stendahl PSD Programme Tutors.
Daniel
Stendahl (right) Private Sector Development (PSD) Programme Tutor says a
word of thanks after being awarded by the 2013 PSD team who graduated
in Dar es Salaam at the weekend and launched a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. Left is Julia Norinder also a PSD programme tutor.
Julia
Norinder (second left) and Daniel Stendahl, Private Sector Development
(PSD) Programme Tutors being awarded by the 2013 PSD team who graduated
in Dar es Salaam at the weekend and launched a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses.
Julia Norinder (second left) and Daniel Stendahl, Private Sector Development
(PSD) Programme Tutors being awarded by the 2013 PSD team who graduated
in Dar es Salaam at the weekend and launched a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses.
Private
Sector Development (PSD) Programme Country focal point, Emmanuel Nnko
shows one of his gifts he received from Tanzania 2013 Private Sector
Development team.
Private
Sector Development (PSD) Programme Country focal points, Saada Mufuruki
(left) and Emmanuel Nnko (second right) being awarded by the 2013
Private Sector Development team
Seasoned entrepreneur Zuhura Muro being awarded by the Tanzania 2013 Private Sector Development team.
Julia
Norinder (second left) Private Sector Development (PSD) Programme Tutor
speaks to guests and participants during the launch of a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- introduced to help local entrepreneurs formalize and grow their businesses.
Ezamo
Maponde, Assistant Director, Private Sector Development in the Prime
Minister's office (left) speaks during the launch of a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to
help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. The
website was a brainchild of Private Sector Development (PSD) Programme
2013 Team from Tanzania. Right standing is Daniel Stendahl PSD Programme
Tutor and seating is seasoned entrepreneur Zuhura Muro .
Ezamo Maponde, Assistant Director, Private Sector Development in the Prime Minister's office (right) speaks during the launch of a new website- www.fanyabiasharatanzania.com- to
help local entrepreneurs formalize and grow their businesses. The
website was a brainchild of Private Sector Development (PSD) Programme
2013 Team from Tanzania. Left is seasoned entrepreneur Zuhura Muro
======= ======= ========
WAJASIRIAMALI wazawa sasa
wanaweza kurasimisha biashara zao kwa urahisi, ziwe ndogo au kubwa,
baada ya kuanzishwa kwa tovuti iliyosheheni taratibu zakufuata pamoja na
hati muhimu za kisheria zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambazo
ujazwa kabla ya kurasimisha biashara.
Tovuti hiyo - www.fanyabiasharatanzania.com –
ni zao la Timu ya Tanzania ya mwaka 2013 katika Programu ya Maendeleo
ya Sekta Binafsi iliyopewa mafunzo na Serikali ya Sweden kupitia shirika
lake la Sida, ikishirikiana na SIPU International na Jarskog Konsult
kwenye masuala ya Mkakati wa Usimamizi wa Biashara na ukuaji wa sekta binafsi.
Akizungumza
wakati wa mahafali na uzinduzi wa tovuti hiyo, Kiongozi wa timu, Dk
Ellen Otaru Okoedion alisema tovuti hiyo imetengenezwa na timu ya
wajasiriamali wakitanzania na wawakilishi kutoka sekta ya umma chini ya
mpango wa PSD, unaolenga kuwasaidia wajasiriamali wazawa na watu wengine
wanaojihusisha na biashara kupata taarifa mbali mbali muhimu
zakuendeleza biashara zao.
"Hii
tovuti itawaokolea muda wao, fedha na nguvu zao katika kutafuta taarifa
ambazo mara nyingi utawanyika, na kutopatikana kwa urahisi na mara
nyingi mjasiriamali ulazimika kutumia gharama kubwa kukusanya taarifa
hizi," alisema.
Uanzishwaji
wa tovuti hiyo ni hatua ya kuhamasisha ukuaji wa biashara ndogo, wakati
huo huo kuunga mkono jitihada za serikali katika kurasimisha biashara
hizo, ambazo uhamasisha si tu biashara kuwa na ushindani ndani ya nchi,
kanda na kimataifa, lakini pia kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi.
Tovuti
hiyo ina taarifa zote muhimu zinazohitajika kuanza, kusajili na kupanua
biashara nchini Tanzania.Pia imeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa
wizara zote muhimu, mashirika na sekta binafsi. Pia imetoa maelekezo ya
jinsi ya kujaza fomu za usajili wa biashara zinatolewa na wakala wa
usajili wa biashara na utoaji leseni (BRELA).
"Fomu
muhimu zakujaza imetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili kuwezesha raia
yeyote kuwa na uwezo wa kuelewa na kujaza taarifa zinazohitajika kwa
urahisi," alisema Dk Ellen Okoedion.
Alisema
kuwa ili kuwafikia watanzania wote, waandaji wa tovuti hiyo wapo
mbiyoni kuiunganisha na huduma za simu za mikononi ili kumwezesha hata
wale waliopo vijijini kuweza kufurahia huduma hiyo.
"Tovuti
hii ni rahisi kuitumia, ikiwa na taarifa juu ya masuala ya biashara,
fursa mbali mbali, kama vile mafunzo ya kutosha, zabuni na maonyesho ya
biashara," alisema kiongozi huyo wa timu.
Kwa
upande wake, Mgeni rasmi, Ezamo Maponde, Mkurugenzi Msaidizi wa
Maendeleo ya Sekta Binafsi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema kuwa ili
kufikia ukuaji wa uchumi, mchanganyiko wa uwekezaji katika makampuni
mbali mbali ya biashara, rasilimali watu wenye ujuzi, miundombinu bora,
mazingira mazuri ya kibiashara na uwekezaji wa kigeni vinahitajika.
“Mafunzo haya yamekuwa na manufaa makubwa na mafanikio katika kukabiliana
na changamoto za maendeleo yetu, ikiwa ni pamoja na haja ya kupata
ukuaji mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi nchini na kupunguza umaskini kwa
ujumla," alisema.
Alitoa
wito kwa vijana wa Kitanzania ambao wana nia ya kuingia katika
ujasiriamali kubadili mawazo yao na kuona ni kama chanzo cha ajira na si
kama ajira ya muda mfupi na kuipongeza Serikali ya Sweden kwa kazi
nzuri wanayofanya katika kubadilisha na kuboresha sekta binafsi nchini.
NA ANKAL ISSA MICHUZI
0 comments:
Post a Comment