Leo February 17 kutoka Mhakama kuu
kanda ya Dar es salaam,msanii wa maigizo nchini Tanzania Elizabeth
Michael maarufu Lulu alikuwa akisomewa shitaka lake la kuua bila
kukusudia msanii mwenzake wa maigizo Steven Kanumba April 07 2012 eneo
la Vatican.
Akisoma maelezo ya awali wakili wa
serikali Monica Mbogo mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo Rose Teemba
amesema mshtakiwa siku ya tukio kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na
mshtakiwa na baadaye mshtakiwa aliondoka usiku wa saa sita baada ya
marehemu kuanguka chumbani ambapo alfajiri ya february 07 majira ya saa
11 alfajiri Lulu alikamatwa eneo la Bamaga.
Kwa upande wake wakili Peter Kibatala
ambaye anamtetea Lulu amesema wameridhishwa na sehemu kubwa ya maelezo
ya awali ya mteja wao, ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka itakapopangwa
tena huku kila upande ukitarajia kuleta madhahdi watatu.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie waliohudhuria leo mahakamani ni Dr.Cheni na Kajala.
0 comments:
Post a Comment