SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, January 4, 2014

RATIBA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DK. WILLIAM MGIMWA

Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa  Enzi za Uhai Wake

 Waziri Mkuu(Sera Uratibu na Bunge) Dk. William Lukuvi
---
Na Kiza Sungura- MAELEZO Dar es Salaam
 
KAMATI ya Taifa inayohusika na mazishi ya aliyekuwa waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa  imetoa ratiba ya mazishi ambapo mwili wa marehemu utawasili siku ya jumamosi tarehe nne saa saba mchana  katika uwanja wa Mwalimu Nyerere  Terminal  II na kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni B jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu(Sera Uratibu na Bunge) Dk. William Lukuvi alisema kamati itakayohusika na mapokezi ya mwili wa marehemu ni ofisi ya Waziri Mkuu  itakayohusika na ndugu, viongozi na wananchi na Kamati ndogo ya mkoa wa Iringa inayoongozwa na mkuu wa mkoa huyo Dk. Christine Ishengoma.

Dk. Lukuvi alisema siku hiyo ya jumamosi saa kumi na moja jioni mwili marehemu utapelekwa katika hospitali ya Lugalo na tarehe tano siku ya jumapili saa tano na nusu asubuhi mwili wa marehemu utapelekwa katika  ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya ibada na kutoa heshima za mwisho.

Alisema ifikapo saa nane mchana mwili wa marehemu Dk. Mgimwa utapelekwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Terminal I kwa ajili ya kuelekea Mkoa wa Iringa.

Ifikapo saa kumi kamili alasiri mwili wa marehemu utakuwa umewasili Mkoa wa Iringa katika uwanja wa ndege Nduli  na kuagwa na viongozi na wananchi wa mkoa huo katika ukumbi wa Siasa kilimo na baada ya hapo utapelekwa kijijini kwake Magunga.

Waziri Lukkuvi alimalizia kwa kusema kuwa shughuli za mazishi ya Marehemu Dk. Mgimwa zitafanyika 6.1.2014 kuanzia majira ya saa sita mchana  katika kijiji cha Magunga mkoani Iringa na atazikwa kwa heshima zote za Kiserikali.

0 comments:

Post a Comment